Makamo wa Kwanza wa Rais , Maalim Seif pamoja na Makamo wa Pili wa Rais
Balozi Seif wakisoma khitma wakiwa katika Maziko ya Bi Kidude Masjid
Mushawwar Mwembeshauri
Mvua iliyokuwa ikinyesha kwa nguvu haikuwazuia watu wengi waliofika shamba Kitumba kwenye maziko ya Bi Kidude
Rais wa jamhuri ya Muungao Dk Jakaya Kikwete akifuatiwa na Rais wa
Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein walipofika Kitumba yalipofanyika maziko
ya Bi Kidude
Umati wa waumini waliohudhuria maziko ya Bi kidude wakitanguliza jeneza la Bi Kidude tayari kwa safari yake kupelekwa Kitumba kwa mazishi
Mwili wa Bi Kidude ukitolewa kutoka kwenye jeneza kwa ajili ya kuhifadhiwa katika kaburi
Vijana waliobeba Jeneza la mwili wa Marehemu Msanii maarufu Fatma Binti
Baraka (kidude) wakati wa maziko yake yaliyofanyika leo huko kijijini
kwao Kitumba,Wilaya ya Kati Unguja, ambapo maziko yake yamehudhuriwa na
wasanii mbali mbali ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika maziko ya marehemu Bi Fatma
Baraka (Kidude) kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Katr Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed
Shein,(kutoka kulia) Rais wa jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete,Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif,na Makamo
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,wakiitikia dua baada ya maziko ya
Msanii maarufu Fatma Binti Baraka (kidude) aliyefariki jana na kuzikwa
leo Kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Katri Unguja.
ZANZINEWS.BLOG PICHA
No comments:
Post a Comment