HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

23 April 2013

JE NI ETHIOPIA AU ? KAGAME CUP


 

Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Juni jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limesema kwamba mashindano hayo yanaweza kufanyika katika nchi nyingine itakayokuwa tayari kufuatia Ethiopia kueleza katika barua yao kwamba wanataka michuano hiyo ifanyike mwezi Septemba.


Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, amesema  kuwa bado suala la udhamini wa michuano hiyo limekuwa tatizo na ndiyo maana wanashindwa kueleza wazi mikakati ya michuano hiyo ya mwaka huu.


Musonye alisema kwamba ili mashindano hayo yafanyike katika ubora wake wa kimataifa, CECAFA inahitaji kiasi cha Dola milioni moja za Marekani.


"Tuko katika kutafuta wadhamini na hadi kufikia mwisho wa mwezi huu tutajua ni nani hasa atakuwa mwenyeji wa michuano hii kwa kuthibitisha kwamba ataweza kuhudumia mahitaji yanayotakiwa. Uenyeji kwa sasa ni wa Ethiopia japo michuano inaweza pia kuhamishiwa katika nchi nyingine," alisema Musonye.


Aliongeza kuwa mashindano ya Kombe la Kagame ni muhimu katika ukanda huu na hayatafanyika zaidi ya mwezi Julai hivyo kama mwenyeji atashindwa kuwa tayari kwa muda huo, michuano inaweza kuhamishwa huku wakiendelea kusaka wadhamini.


Awali nchi za Sudan na Rwanda ziliandika barua ya kuomba kuwa wenyeji wa michuano hiyo ya kila mwaka lakini bado vyama vya soka vya nchi hizo havijathibitisha kama vimeshapata udhamini wa kusaidia gharama za maandalizi.


Yanga ndiyo bingwa mtetezi wa michuano hiyo ambapo pia mwaka huu Simba itashiriki kutokana na kuwa bingwa wa Tanzania Bara msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers