Anna Kibira ambaye ni mchezaji wa zamani wa kiongozi na muda mrefu
ambaye mchango wake kwenye mchezo upo wazi, na Mbunge wa Afrika
Mashariki Shy-Rose Bhanji leo watapigiwa kura kuchagua mwenyekiti wa
chama cha netiboli, Chaneta, Dodoma.
Wagombea hao walipitishwa katika usaili wa wagombea uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma chini ya kamati ya uchaguzi iliyoongozwa na Betty Mkwasa.
Wagombea wengine waliopitishwa katika usaili huo ni wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti: Zainabu Mbiro na Agnes Mangasila, wakati nafasi ya mweka hazina ni Agnes Hatibu. Betty Mkwasa amesema wagombea wote wametimiza vigezo vilivyotakiwa kwenye fomu ya uchaguzi mkuu, jambo ambalo halikuwa kikwazo katika usaili.
Mkwasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma aliwataja wagombea wa nafasi ya ujumbe ambao wamepitishwa kwenye usaili kuwa ni Yasinta Silvester, Mwajuma Kisengo, Mary Protas, Rose Kisiwa, Judit Ilunda, Hilder Mwakatobe, Penina Igwe, Asha Sapi na Fotunata Kabeja.
"Hawa ndio wagombea watakaopigiwa kura katika uchaguzi mkuu," alisema Mkwasa.
Naye kaimu katibu wa CHANETA anayemaliza muda wake Rose Mkisi alisema mikoa iliyowasilisha wajumbe kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi huo ni Dar Es Salaam, Kagera, Pwani, Mbeya,Dodoma, Manyara, Mwanza na Katavi.

No comments:
Post a Comment