Kocha wa Cardiff akishangilia na mashabiki |
Cardiff City imekuwa timu ya kwanza kujihakikishia nafasi ya kupanda daraja la ligi kuu soka nchini England msimu ujao licha ya sare ya bila kufungana na Charlton Athletic katika mchezo wa usiku huu.
Pointi moja waliyoipata, iliwatosha kabisa
kuwafanya wawe miongoni mwa timu 20 zitakazo pambana msimu ujao kusaka
ubingwa wa kombe la ligi kuu nchini England,ligi yenye mashabiki wengi
duniani.
Hii
imekuwa mara ya kwanza kwa Cardiff kurejea kwenye ligi ya juu zaidi
nchini Uingereza baada ya miaka 51 ya kupambana kwenye ligi ndogo toka
waliposhuka daraja mwaka 1962.
Cardiff inakuwa timu ya pili kutoka nchi ya
Wales ambayo ni sehemu ya Taifa la Uingereza kushiriki ligi kuu baada ya
Swansea iliyopanda daraja misimu miwili iliyopita. Pia inakuwa timu ya
46 tofauti kushiriki ligi kuu nchini England toka ilipoitwa ligi kuu ya
England mwaka 1992.
Misimu mitatu iliyopita,Cardiff ilijitahidi
kupanda daraja lakini ilijikuta ikishindwa baada kutolewa kwenye michezo
ya mtoano,lakini msimu huu umekuwa wa mafanikio kwa klabu hiyo ambayo
inanolewa na kocha Malcolm George kutoka Scotland .
Mmiliki wa klabu ya Cardiff,Vincent Tan |
Miaka mitatu iliyopita,wiki chache baada ya kufungwa na Blackpool na
kupoteza nafasi ya kwenda ligi kuu,Cardiff ilijikuta kwenye matatizo
makubwa baada ya kufikishwa mahakamani mara tatu baada ya kushindwa
kulipa deni la malimbikizo ya kodi. Lakini deni hilo lilikuja kulipwa
lote kwa pamoja na Bilionea Vincent Tan kupitia kampuni yake ya
Malaysian Consortium ya Malaysia,ambayo iliwekeza kiasi cha paundi
milioni 60 kwenye klabu hiyo.
Timu nyingine zitakazopanda daraja msimu ujao
kwenye ligi ya Uingereza na zile zitakazoshuka kutoka ligi kuu kwenda
ligi ya chini zitajulikana mwishoni mwa mwezi ujao.
No comments:
Post a Comment