MARA
baada ya kuchukua fomu za kutaka kugombea nafasi ya urais wa Chama cha
Soka Zanzibar (ZFA), Ibrahim Dharamsi Raza, amesema dhamira yake kuu ni
kuiondeshea Zanzibar aibu inayotokana na kushuka hadhi kisoka.
Raza
aliyechukua fomu hiyo jana katika ofisi za Kamati ya Uchaguzi ya ZFA
iliyoko uwanja wa Amaan, alisema hafurahishwi na kuzorota kwa mchezo
huo, hali inayowakimbiza mashabiki viwanjani.
Akijibu
masuala ya waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hiyo, Raza
aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa mamlaka za michezo
ikiwemo Makamu Mwenyekiti wa ZFA (1995-2000), alisema soka la Zanzibar
limekosa uongozi makini na wenye uchungu wa kuliokoa.
"Inasikitisha
kuona ni watu wachache sana wanaokwenda kuangalia mechi za ligi siku
hizi, tafauti na zamani ambapo viwanja vya Amaan na Mao vilikuwa vikijaa
na watu wakifurahika", alisema Raza.
Alisema
iwapo atafanikiwa kushinda katika kinyang'anyiro hicho, anakusudia
kushirikiana na viongozi wenzake na wadau wote wa soka nchini, kupanga
mikakati madhubuti ili wanamichezo warejeshe imani kwa ZFA ambayo
imepotea kutokana na uongozi usiojali maslahi ya umma na kuweka mbele
ubinafsi. Aidha,
alisema lengo jengine ni kuhakikisha ZFA inaimarisha uhusiano wake na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na hivyo kudai mgao na haki zake
zinazotokana na misaada ya FIFA kupitia mgongo wa TFF.Mgombea
huyo alisema, uongozi wake utakuwa wa pamoja kati ya Unguja na Pemba,
akieleza kuwa bila ushirikiano kati ya pande hizo maendeleo yatakuwa
ndoto.Uchaguzi
mdogo wa ZFA kujaza nafasi ya urais iliyoachwa wazi na Amani Ibrahim
Makungu aliyejiuzulu mwishoni mwa mwezi Januari, unatarajiwa kufanyika
Juni 8, mwaka huu katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani.
No comments:
Post a Comment