HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 May 2013

MABONDIA WAPATA AHUENI YA KOUNGEZEWA MUDA WA MAZOEZI


 

Wakati mashindano ya ngumi ya Majiji yakisogezwa mbele, Shirikisho la mchezo huo Nchini (BFT) limewataka mabondia wa hapa nchini kutumia nafasi hiyo kujiimarisha ili waweze kufanya vizuri katika mashindano hayo yatakayoshirikisha klabu kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Mashindano hayo sasa yatafanyika kuanzia Julai Mosi hadi 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza.

Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga, amesema makocha wa timu hizo wanapaswa kutumia nafasi hiyo kuongeza programu za mazoezi ili wachezaji wawe imara na tayari kutoa ushindani kwa wapinzani wao.

"Makocha mnapaswa kutumia fursa hii kwa faida ya kuongeza mafunzo kwa mabondia, kama wenyeji tunatakiwa kuhakikisha tunaongoza kunyakua medali " Mashaga alisema.

Aliyataja majiji ambayo yamethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Arusha, Mbeya, Dar es Salaam, Tanga, Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura na wenyeji Mwanza huku akisema pia wametoa mialiko kwa timu za Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers