HUKU
wakikanusha ripoti za awali zinazoendelea kusambaa juu ripoti ya kifo
cha msanii Albert Mangwea, Kamati ya Mazishi ya msaniii huyo, imesema
kuwa inatarajia kuuleta mwili wa marehemu huyo kesho kama ilivyopangwa
na kuuaga Jumapili katika Viwanja vya Leaders Club, baada ya kulala
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa siku moja.
Marehemu Mangwea
Mangwea
moja ya wasanii nyota hapa nchini alifariki nchini Afrika Kusini na
kuzua huzuni kubwa kwa wadau wa muziki na Watanzania kwa ujumla, hasa
kutokana na umahiri wake kwenye kazi hiyo, huku kifo chake kikipokelewa
kwa masikitiko makubwa mno na redio zote kusikika mara kwa mara nyimbo
zake zikipigwa kama sehemu ya kuomboleza msiba wa msanii huyo nyota.
Mara
baada ya kuwasili kesho, mwili wa marehemu utafikia kwanza katika
Hospitali ya Muhimbili huku siku inayofuata ratiba zilizopangwa
kuendelea kwa ajili ya kuustili mwili wake.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Kamati iliyoundwa ya kuratibu
shughuli zote za msiba huo, Adam Juma, alisema kuwa maandalizi kwa ajili
ya kuleta kwa mwili huo na utaratibu mzima wa maziko yake yanaendelea.
Alisema
ili waweze kufanikisha suala hilo, wanaomba msaada wa Watanzania bila
kubaguana kwa namna yoyote, maana Ngwea alikuwa mtu wa watu, hivyo
hakuna haja ya kuleta propaganda katika suala hilo.
“Tunakabiliwa
na changamoto nyingi katika msiba huu, hivyo tunawaomba Watanzania
wenzetu waweze kuchangia kwa namba ya Vodacom, 0754 074323 au Tigo 0658
074324 ambazo fedha zote zitaingia kwenye simu za kaka wa marehemu,
Kenneth Mangwea, ambaye ni kama mwenyekiti katika Kamati hii ya kuratibu
mazishi ya msanii huyu.
“Kuna
vitu vingi vya kufanya na vyote vinahitaji gharama, kama vile kuleta
mwili wake, kuuaga sambamba na usafiri wa ndani, bila kusahau safari ya
kuelekea Morogoro kwa ajili ya maziko yake,” alisema.
Aidha,
Kamati hiyo inayoongozwa na Shirikisho la Muziki Tanzania, chini ya
Rais wake, Addo Novemba, ilisema kuwa ripoti iliyoanza kutolewa jana
kwenye mitandao ya kijamii si ya kweli.
“Tunaomba
Watanzania tuendelee kuwa na subira katika suala hili, maana ripoti
iliyosambazwa kwenye mitandao si ya kweli na imeletwa kwa ajili ya
kumdhalilisha marehemu Ngwea,” alisema Novemba.
Msiba
wa Ngwea umepokelewa kwa masikitiko makubwa na Watanzania, hasa
kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya,
maarufu kama Bongo Fleva, akitamba na nyimbo nyingi, kama vile Gheto
Langu, Mikasi, Speed 120 na nyinginezo lukuki.
Aidha,
mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva nchini, P-Funk, amefunga mdomo
kuelezea kwanini aliamua kuwapiga marufuku redio ya Clouds FM kucheza
nyimbo alizorekodi yeye na kuimbwa na marehemu Ngwea enzi za uhai wake.
"Kwa
sasa sitaki kusema lolote juu ya nyimbo hizo za Ngwea kuchezwa au
kutochezwa Clouds FM," alijibu kwa kifupi akiwa na maana ya kuelekeza
akili yake kwenye msiba wa msanii Ngwea.
No comments:
Post a Comment