Mchezaji wa kimataifa wa uganda Uganda Cranes Moses Oloya huenda akatua nchini muda wowote kutoka sasa akiwa mbioni kujiunga na simba.
Simba ambao msimu huu wameshindwa kutetea ubingwa , wanajiandaa na michuano ya Cecafa Kagame Cup, iliyopangwa kuafanyika
Sudan Mwezi ujao .
Timu hiyo bado inajiandaa kwa msimu ujao na bado inatafuta wachezaji wengine baada ya winga wao machachari Mrisho Ngassa ambaye amejiunga na mabingwa wapya wa ligi ya Tanzania Yanga.
kamati ya simba ya usajiri inayoongozwa na Zacharia Hanspoppe amethitisha kuwa majadiriano yanaendelea mchezaji huyo pia yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya cranes
Oloya, -ambaye ni mchezaji wa Saigon Xuan Thanh kutoka Vietnam,Mchezaji huyo atajiunga na simba baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Libya na ile ya kuwania kufuzu kombe la dunia mwezi ujao .
sasa ataungana na mchezaji mwenzake Samuel Ssekoom mchezaji wa zamani wa (URA) ambaye naye amesaini kuchezea klabu hiyo .
Simba sasa inawachezaji watano wa kigeni na hii ina maana kuwa watatakiwa kupunguza baadhi ya wachezaji ili kutimiza sheria ya wachezaji wa tano wa kimataifa wachezaji hao ni pamoja na Mlinda mlango Abel Dhaira (Uganda), Felix Sunzu (Zambia) na Mude Mussa kutoka Uganda.
Timu hii tayari imeshamaliza kazi ya kusajiri beki Issa Rashid, Mlinda mlango
Andrew Ntalla, Mshambuliaji Zahor Pazi na kiuongo Twaha Shekuwe.
No comments:
Post a Comment