Michuano ya Kombe la Taifa inayoshirikisha timu za
mikoa ya Tanzania (Taifa Cup) haitafanyika tena mwaka huu kutokana na
sababu za ukosefu wa fedha, imeelezwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema
kuwa wameshindwa kupata wadhamini wa michuano hiyo na hivyo
haitafanyika.
Hata hivyo, Wambura aliongeza kuwa mashindano hayo yatafanyika
mwakani baada ya kukamilika kwa mazungumzo yao na kampuni iliyojitokeza
kuidhamini.
"Hatutakuwa na Taifa Cup mwaka huu kwa sababu hatuna fedha za
kulipia gharama za usafiri na malazi ya timu shiriki. Mwakani tunaamini
itafanyika kwa sababu tuko katika mazungumzo na kampuni ambayo
imejitokeza kudhamini michuano hiyo," alisema Wambura bila kuitaja
kampuni hiyo.
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa mashindano hayo kutofanyika kutokana na kutopata wadhamini.
No comments:
Post a Comment