Timu ya taifa ya soka za Taifa za Malawi na Kenya zimetoka sare kwa kufungana mabao 2-2 mjini Blantyre katika mechi ya kufuzu kombe la dunia.
Malawi walikuwa wanaongoza mabao mawili kwa moja
lakini katika dakika ya mwisho Chimango Kayira alijifunga na kupunguza uwezekano wa Malawi kusonga hatua
inayofuata.
The
Flames ndio waliowakwanza kupata bao katika dakika ya 46, bao lililofungwa na
Robion Ngalande, lakini dakika sita baadaye Mohamed Jamal akaisawazishia
Harambee Stars.
Katika dakika ya 81, Robert Ng'ambi alifunga bao
la pili la Malawi, kabla ya Kayira kujifunga na mechi kumalizikia
mabao mawili kwa mawili.
Matokeo hayo yana maana kwamba mabingwa wa
Afrika Nigeria ndio watakaofuzu hatua inayofuata kutoka kundi la F,
ikiwa wataishinda Namibia mjini Windhoek, mechi inayochezwa baadaye
usiku huu.
Hdi kufika kuna bakia mwaka mmoja , kabla ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kuanza nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment