Mchezaji nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar ameiondoa uingereza kama timu inayoweza kushinda kombe la dunia mwakani litakalo fanyika Brazil .
Mchezaji huyo wa Santos ambaye anaondoka msimu huu na kujiunga Barcelona anajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu inayoongozwa na Roy Hodgson's katika Dimba la Maracana kesho jioni .
Japokuwa amekubali uingereza inawachezaji wazuri lakini akasema wamefanya vizuri kwenye klabu zao na sio timu ya taifa ,Aamini kama wanauwezo wa kushinda michuano mikubwa kama hiyo kwani wanapocheza katika timu ya taifa hawachezi kama vilabuni .
Akizungumza na Gazeti la The Sun, Neymar : "Nina heshimu wachezaji wa uingereza wamejitahidi sana katika vilabu vyao ."Lakini katika timu ya taifa, siitazamii uingereza kabisa na nadhani watakwenda kuwa mdebwedo kabisa katika kombe la dunia.
"Tunataka kushinda kombe la dunia mbele ya mashabiki wa nyumbani na timu ambazo hazitakuwa Mdebwedo ni uispania na Ujerumani .
"Baada ya hapo natazama kundi la timu aina ya Argentina, Holland, Italy na timu nyingine moja au mbili zaidi . Lakini Uingereza siifikilii kabisa "
No comments:
Post a Comment