Vilabu vinne ambavyo vilihusika na njama ya kupanga matokeo ya mechi vimepigwa marufuku nchini Nigeria.
Katika mechi moja klabu moja iliilaza nyingine magoli 79-0 na magoli 67-0 katika mechi ya pili.
Jumla
ya magoli 146 zilifungwa katika mechi hizo mbili, idadi ambayo inaingia
katika vutabu vya kumbukumbu kama mechi iliyokuwa na idadi kubwa zaidi
ya magoli duniani.
Klabu ya Plateau United Feeders iliilaza timu ya
Akurba ili hali timu ya Polisi ya Machine FC kwa upande wake ikailaza
Bubayaro magoli 67-0.
Mwenyekiti wa kamati andalizi ya shirikisho la
mchezo wa soka nchini Nigeria, Muke Umeh amesema ufisadi na ulaghahi wa
kiwango hicho hakiwezi kukubalika katika soka ya sasa.
Umeh ametangaza kuwa baada ya mkutano wa kamati
hiyo, ilibainika wazi kuwa vilabu hivyo vina kesi ya kujibu na hivyo
vyote vinne vimepigwa marafuku ya kushiriki katika mecho yoyote, hadi
uchunguzi utakapokamilika.
Mchezo unaopendwa na wengi
Kabla ya mechi hiyo vilabu vya Plateau United
Feeders na Police Machine vilikuwa na alama sawa na vilikuwa vikipania
kupandishwa daraja hadi ligi daraja ya pili.
Feeders ilipata magoli 72, katika kipindi cha
pili ili hali Machine nao wameripotiwa kufunga magoli 61 katika kipindi
cha mechi yao.
Kufuatia matokeo hayo Plateau ilimaliza ya
kwanza kwenye msimamo wa ligi na idadi kubwa ya magoli ikifuatwa na timu
hiyo ya polisi.
''Tutachunguza sakata hii na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika'' Alisema Ummeh.
Mkurugenzi wa michezo na mashindano wa
Shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, Dkt. Mohamed Sanusi,
amekariri tangazo lililotolewa na mwenyekiti wa kamati andalizi kuwa
waliohusika wataadhibiwa vikali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NFF, vilabu
vilivyohusika, wachezaji,, maafisa wa kiufundi wa timu na wasimamizi wa
mechi hiyo watakaopatikana kuhusika kwa njia moja au nyingine, katika
kashfa hiyo ambayo imetajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya soka
nchini Nigeria watachukulia hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment