HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 March 2013

JUMA NKAMIA :HUENDA RAGE AKAWA NDIO TATIZO SIMBA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhk4WZYuXxNnVRUdP7A4IAYyPS9yoQklEMfJkHU_QozSIqFi3BCEjWIOBNT1gyaIBiCKpagyHul2xYsubTcwiBAnFOY0lvip9LYz9YXSzYUXxoqqNFtuGBY-P3nEsDQgUFkiX4SjMM4PCg/s1600/Juma-Nkamia.jpg
Aliyewahi kuwa katibu mwenezi wa klabu ya Simba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kondoa kusini Juma Selemani Nkamia amesema kujiuzulu kwa viongozi wa klabu ya Simba ni pigo kwa klabu hiyo na kwamba kuna haja ya mwenyekiti wa klabu hiyo kutafakari juu ya mustakabali wa klabu hiyo haraka iwezekanavyo.
Akiongea na Rockersports Nkamia amesema habari za kujiweka pembeni kwa viongozi hao mjumbe wa kamati ya utendaji ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zakharia Hans Poppe na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geoffrey Nyange Kaburu zimemshitua sana na kwamba huenda kunasababu iliyojificha nyuma ya pazia na kwamba kuna haja ya kuketi chini na kutafakari kwa kina.
Amesema Has Poppe amekuwa na mchangano mkubwa katika klabu ya Simba tangu wakati ule akiwa ni kiongozi wa klabu hiyo na kwamba huenda kuna tatizo kubwa ambalo kiongozi huyo ameliona na kuona bora akae pembeni jambo ambalo linatahitaji tafakari ya kina ya wanachama.
Nkamia amesema huenda tatizo likawa ni kwa mwenyekiti wa klabu hiyo kupingana na maamuzi ya vikao halali vya wajumbe wa kamati ya utendaji au kujiamulia mambo yake mwenyewe  hali ambayo huenda ikapelekea wajumbe wengine wakafuata nyayo hizo na kuleta athari kubwa kwa klabu hasa wakati huu ligi ikiwa inaelekea ukingoni.
Amemuomba mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaji Ismail Aden Rage kufanya busara kwa kulitazama jambo hili kwa makini sana kwani huenda yeye akawa ndiyo tatizo ndani ya klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers