Mtihani wa uwakala wa wachezaji (players agent) na uwakala wa mechi (match agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Septemba 26 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa
ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya
Kiingereza ambayo ni moja kati ya lugha nne rasmi za FIFA wanatakiwa
kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani ambapo watapewa utaratibu
na maeneo ambapo mtihani huo unalenga.
Mtihani huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi, na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.
Mpaka
sasa Tanzania ina mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA.
Mawakala hao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf
Bakhresa na Said Tully.
No comments:
Post a Comment