Luis Suarez Anatakiwa kubaki Liverpool na kutupilia mbali offa ya kwenda kucheza katika klabu ya Arsenal, Hii ni kauli ya Mchezaji na mshambuliaji wa zamani wa washika Bunduki Ian Wright.
Liverpool imekataa offa mbili zilizotolewa na klabu ya Arsenal kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 26-, ambaye anataka kucheza ligi ya mabingwa ulaya.
"Nitamkaribisha Arsenal kwa mikono yangu yote miwili," Wright ainaiambia BBC Sport.
"Lakini ningekuwa Suarez, na ukitazama vitu vyote pale,Haionyeshi kama kuna jambo la umuhimu wa yeye kwenda Arsenal. Ningempa nafasi moja zaidi kubaki Liverpool ."
Wright, ni moja kati ya watangazaji wa kipindi cha mpira wa miguu cha BBC Radio 5 live's sambamba na Kelly Cates, anaongeza : "Arsenal sasa imeamua kuamka na kushindania majina makubwa na bila kufanya hivyo itaachwa nyuma."
Mshambuliaji huyo amesha sema kuwa Angependa kuondoka Anfield
japokuwa amesaini kandarasai ndefu mwaka 2012 Mwezi August .
Anaamini kuwa offa ya karibuni iliyotolewa na
Arsenal's ya pauni £40m jumlisha £1 kama ushawishi inamrushusu yeye kuanza kuongea na klabu nyingine,Lakini Liverpool aionyeshi kuwa wanataka kumuuuza mchezaji huyo mpaka itakapo fika kitita cha £50m-.
Huku Liverpool ikiwa haijacheza michuano ya Ligi ya mabingwa Barani ulaya Tangu 2009, Arsenal itakuwa inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kumi na saba mfululizo .
Wright anadhani kuwa hata kama wakimleta Suarez, Bado majina makubwa yanahitaji kuletwa .
"Tunahitaji kuona mambo ambayo hatujayaona kwa muda mrefu kidogo na wanatakiwa kufanya hivyo kama wanavyofanya Manchester United, Manchester City , Chelsea ," .
"Lakini sidhani kama wako ndani ya wakati kwa sababu , kwa sasa,wanahitaji kufanya kazi ya ziada kwa hawajashinda kitu chochote kwa muda mrefu .Hii ndio sababu Arsenal kuwa katika hari ya hatari.
"Ningependa kuwaona wakienda mbali zaidi kuhusu
Suarez, lakini hawawezi tu kumnunua yeye na timu nzima kubaki vile vile . Nadhani wanahitaji Mlinda Mlango ,Walizini wawili wa kati, walinzi wa kulia na kushoto - Viungo wengine na washambulizi wawili.
" Haita leta maana kwa kumsainisha Suarez kwa pesa hiyo na kuacha kufanyika marekebisho nafasi nyingine ."
No comments:
Post a Comment