Wiki hiii kumeibuka sakata la Mwinyi kazi moto kuripotiwa kutoroka kambini wakati timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Taifa stars ikiwa inajiandaa kucheza mechi ya marejeano ya kuwania kufuzu fainali ya michuano ya CHAN inayohusisha timu za taifa ambazo wachezaji wake wanacheza ligi ya ndani dhidi ya Uganda Cranes mechi itakayo pigwa Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.
Bado haijafamika kama mchezaji mwinyi kazi kama atakuwepo au kutokuwepo kwenye mchi hiyo baada ya kuripotiwa kutoroka kambini. Lakini jambo pekee ambalo leo nataka kuwauliza wadau wa soka kuhusu kutoroka kwa mchezaji ambaye kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa shirikisho la soka la Tanzania Angetile Osiah anasema kuwa Mwinyi kazi moto ni mchezaji muhimu kuliko wakati mwwingine wowote sipingani naye kuhusu hilo kwa sasa ! Unajua katika fani ya uandishi wa habari kuna kanuni inayomuongoza mwandishi wa habari ambayo ni 5Wna1 H .
ya Kwanini?lini?wapi?nani?nini?na ilikuaje
Maswali haya tayari wadau wa soka wamekwisha jiuliza kuwa imekuaje jambo hili limejitokeza lakini bila kupata majibu sahihi na ya Msingi kwa waliowengi inawezekana au tukawa hatujui kuhusu utaratibu wa kutafuta visa za kuingia nchi isiyokuwa ya kwako hasa kwa kundi la watu au timu lakini kitu kikubwa hapa cha kujiuliza wachezaji wa stars wapo kambini na pindi wawapo kambini inamaana wapo chini ya Tff ambao ndio wasimamizi wakuu wa timu ya taifa ya Tanzania.
Twende mbali kidogo timu inapokuwa na safari wiki moja baada ya mechi ya nyumbani inayofuata ni ya ugenini kwa ufahamu wetu pass za kusafiria huwa zinakuwa mikononi mwa tff je Kazi moto alifanikiwa vipi kupata pass yake ya kusafiria wakati yupo kambini au kwa maana nyingine tunaweza kupata majibu haya alipoingia kambini hakukabidhi pass yake au timu nzima haikufanya hivyo lakini kwanini linatokea jambo kama hili kwa mara nyingine kuna wakati mchezaji aliwahi kuingiza kimada kambini, ukiacha hilo, Mchezaji mwingine kutoroka na kwenda kutia kandarasi na klabu fulani ya ligi Tanzania , Leo moto katoroka inaonesha kuwa Timu ya taifa ya Tanzania ina ulinzi hafifu mbona wachezaji hawa hawafanyi ujinga huu klabuni kwao ?
Au ni kuwaahadaa waganda kwakuwa wanajua kuwa Kazimoto ndio kila kitu ili wajue hayupo wakati yupo Je mmekwisha wasiliana na familia yake kujua alipo? Mmekwisha ripoti polisi kama haya hayaja fanyika huu utakuwa unafiki wa kutuhadaa watanzania kuwa Kazimoto katoroka na kama ni kweli uzembe huu ni wa nani wa mchezaji huyu kutoroka mbona mambo mengine tunajitia aibu katika taifa! Bado haituingiii akilini alipata vp pass ya kusafiria ?
Je tukisema kuwa yapo mengi yanayofanyika ndani ya kambi ya taifa stars sema hayajapata kutokea hadharani mtatukatalia Haya ni yale ambayo yanasemwa hadharani je yasiyosemwa Tunaomba mpunguze kadhia hii ya kutuaibishiaa timu yetu ya taifa tumechoka kwani yapo ya kusema hadharani lakini siyo haya Tff kweli hamjui ?
na inawezekana katibu hajui basi yupo anayejua kwa sababu haiwezekani kuwe hakuna mtu asiyefahamu jambo kubwa kama hilo ?
na inawezekana katibu hajui basi yupo anayejua kwa sababu haiwezekani kuwe hakuna mtu asiyefahamu jambo kubwa kama hilo ?
TFF mna la kutuambia kuhusu uzembe huu
No comments:
Post a Comment