Kocha wa timu ya soka ya taifa ya uingereza Roy Hodgson anategemea kuwa mshambuliaji wake Wayne Rooney ataweka matatizo ya klabu yake pembeni katika mechi ya kirafiki dhidi ya uskochi jumamatano ijayo . Kuna fununu nyingi kuhusu mustakbari wa mchezaji huyo katika klabu yake ya
Manchester United na kijana huyo mwenye miaka 27-amekosekana katika mechi za maandalizi katika ziara ya united kutoakan na majeruhi .
"Akiri yake imetulia," Anasema Hodgson. "anaweza kuitumikia klabu na timu ya taifa ,Kitu ninacho tegemea kwa wachezaji wote.
"Wachezaji hawawezi kuleta matatizo ya timu zao kwenye timu ya taifa ."
Aliongeza : "Kama wangekuwa na matatizo kwenye timu ya taifa vile vile hawawezi kuyapeleka kwenye klabu zao ni vitu viwili tofauti .
"Nina tegemea wachezaji wakija , hapa [Kujiunga na timu ya taifa na alihudhiria mechi moja ya maandalizi ya msimu ambayo haikuhudhuriwa na Mashabiki Dhidi ya Real Betis - katika kujiandaa na msimu mpya wa ligi 2013-14 .
Amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya msuri na Bega,huku Manchester united ikiwa imekataa offa mbili kutoka Chelsea
kwa mshambuliaji huyo anayeonekana hajatulia.
Rooney, amecheza mechi 83 akiwa na timu ya taifa ya uingereza na amefunga magoli 36 ,na hakuwemo kabisa katika mchezo wa Ngao ya hisani dhidi ya Wigan
katika Dimba la Wembley siku ya Jumapili, Japokuwa amefanya mazoezi yote na timu ya taifa ya uingereza Leo hii .
Kocha wa United David Moyes anaamini kuwa
Rooney atakuwa fiti pindi atakapocheza zaidi na timu ya taifa ya uingereza Dhidi ya Uskochi .
Na ,alipoulizwa je Rooney atakuwa tayari kucheza mechi hiyo , Hodgson : "Nadhani.
"Tutaona Jumanne itakavyokuwa baada ya mazoezi ya jumatatu Kwa sababu inaweza kuwa hatari zaidi kwani hajakaa sawa tangu apate majeruhi .
"Kama kuna tatizo ,na akafanya mazoezi vizuri , Tutazungumza naye na kufanya maamuzi .
"Kama aanze au aingie baadae , na tutakuwa tayari tunajua na tunatumaini kuwa atakuwa tayari [Katika mechi za kufuzu kombe la dunia ]Mechi zitakazo anza Mwezi Kenda na October."
No comments:
Post a Comment