Na Mwandishi Wetu
:WAKALI wa muziki wa dansi nchini Extra Bongo 'Next Level Wazee wa
Kizigo' keshokutwa Alhamisi wanatarajiwa kuwatambulisha wanenguaji wake
wapya wawili iliyowatwaa kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa
Congo (DRC) katika onyesho maalumu litakalofanyika katika Ukumbi wa
Mamaz & Papaz Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, msemaji wa bendi hiyo, Juma
Kasesa, amesema, kuchukuliwa kwa wanenguaji hao ni sehemu ya mkakati wa
Extra Bongo kuzidi kuimarisha safu yake ya unenguaji inayoongozwa na
mkongwe Super Nyamwela na Otilia Boniface.
Amesema onyesho hilo litakuwa ni maalumu kwa wakazi wa Kigamboni na
vitongoji vyake kuona shoo mpya za bendi hiyo zikichagizwa na ujio mpya
wanenguaji hao ambao wametokea katika bendi ya Wenge Maison Merre ya
Werrason Ngiama Makanda na kwa mwanamuziki Ferre Gorra.
Aliwataja wanenguaji hao kuwa ni Jolie Kindu aka Mrisho Ngassa na Fatuma
Grace aka John Bocco ambao mara baada ya onyesho hilo watatambulishwa
Ijumaa ndani ya Ukumbi wa Eliada Port View Pugu kwa Mjomba huku Jumamosi
zoezi hilo likiendelea ndani ya kiwanja chao cha nyumbani Meeda Club
Sinza na kuhitimisha Jumapili kwenye bonanza lao ndani ya jumba la
maraha Dar West Park Tabata.
Aliwataka mashabiki na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushuhudia
staili na nyimbo mpya za bendi hiyo kama 'Hafidhi' utunzi wa Athanas
Muntanabe, 'Mgeni' Khadija Mnoga 'Kimobitel' na 'Wanawake' wa Papii
Catalogie.
No comments:
Post a Comment