HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 September 2013

FRAT :WAAMUZI ZNZ /BARA KUCHEZESHA LIGI KWA MABADILISHANO



Mwenyekiti wa chama cha wa waamuzi Tanzania FRAT  Said Nasor Amesema kuwa watakaa na shirikisho la soka la Tanzania Tff ili waweze kukaa na ZFA na  kuanzisha mahusiano ya kubadilishana uzoefu, Said Nasor amesema maneno hayo alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Televisheni Cha Star Tv Cha mwanza katika mazungumzo yahusuyo michezo .

Nasor anasema kwa sasa inabidi washirikiane katika sekta ya waamuzi kwani ni jambo la kuinua michezo kwani kwa sasa tayari baadhi ya wachezaji wa Visiwani hucheza katika ligi ya Bara na wale wa Bara hucheza katika ligi ya Visiwa kwa hiyo hipo haja ya kuanza kuboresha maeneo kadhaa ya katika sekta ya uamuzi kwani imekuwa ikirudi nyuma sana hasa katika swala waamuzi ambao wamekuwa wakilaumiwa mara nyingi pindi mambo yanapokwenda hovyo kiwanjani .
Said Nasor anaongeza kwa kusema katika hari ya kiuchumi waamuzi ndio hawathaminiki kabisa kwani wao huonekana bora siku ya Mchezo na Mchezo ukiiisha salama nyakati Nyingi hata posha hawapati kama hari hii ipo Bara vp kwa wenzetu wa Visiwani ambapo kwa udhamini ni tabu .

Aidha ameishauri tff kutazama vizuri katika utoaji wa adhabu pindi kunapoonekana kufanyika makosa kwani hutoa adhabu za kukomoa zaidi kwani kumfungia mwamuzi mwaka mzima sio kitendo cha kiiungwana hata Kidogo ni kushusha kiwango cha Mwamuzi .

Kwa upande mwingine Mwamuzi aliyefungiwa maisha kujihusisha na maswala ya soka Othaman Kazi amesema kuwa Moja kati ya mambo muhimu zaidi katika soka hasa Mwamuzi anapokosea kumfungia mwaka mzima ni uonevu wa hari ya juu hata jirekebishaje wakati hachezeshi mwaka mzima ni kumuonea kijana huyu hapo alikua anazungumzia swala ya Kufungiwa kwa Mwamuzi Martin Saanya Askari Magereza kutoka Morogoro .

"Kwakweli ni mambo ya kusikitisha kumfungia mwamuzi mwaka mzima kitu ambacho kilitakiwa ni kumpa jaribio la mechi nyingine ili muweze kutathmini uwezo wake sio kumfungia kwa kumfungia kwani mnapoteza mambo mengi sana kwanza hachezeshi pili atakosa hata mazoezi na adhabu nzuri ni kumshusha achezeshe mechi za ligi Daraja la chini ili kuona ni makusudi au bahati mbaya "

Aidha Said Nasor amesema kuwa yeye atakaa na viongozi wa vyama hivi vya soka ili kuweza kutazama hata namna ya udhamini sio Vilabu tu kufaidika na Azam tv Bali hata waamuzi.  


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers