Wanasema siku ya mwisho imeboa ... Baada ya wakati wa kiangazi kutawaliwa na Fununu nyingi za usajiri na baada ya Kumalizika kwa uhamisho wa kishindo -Toka Gareth Bale Hadi Luis Suarez, Wayne Rooney Hadi Marouane Fellaini -Dakika 60 za mwisho zimesababisha kugeuza kabisa maoni ya kuwania Ubingwa wa Ligi ya Uingereza .
Makocha wamepigana katika karatasi zao hadi majira ya saa saba usiku kwa saa za Tanzania na Saa nne usiku wa muda wa uingereza hasa GMT na saa Tano usiku kwa saa za kiangazi Uingereza Yaani BST Ulikuwa usiku wa kuamkia Jumanne pale ambapo muda ulipoonekana kuwa Mdogo, Huku baadhi ya hamisho zikifanyika kabla ya Dirisha kufungwa .
Dakika 60 Toka saa 10.30pm hadi 11.30pm kulitokea Hamisho tatu kuu katika ligi ya uingereza ambazo zilikuwa na kizungumkuti ndani yake -Huku nyingine zikiwa na mizani sawa -na zinaweza badili simulizi za ligi ya uingereza msimu huu .
Arsene Wenger aliachana na Tabia yake ya ubahiri baada ya kutoa Pauni za Kiingereza Mil 40 na Kuvunja Rekodi ya Klabu hiyo £42.5 baada ya kumsainisha kiungo wa Real Madrid’s Mesut Ozil.
Mjerumani huyo ametia kandarasai ya miaka Minne huku akipokea ujira wa pauni laki moja na Arobaini kwa juma japokuwa PSG walitaka kuaharibu sherehe lakini kijana huyo alielekea katika viunga Emirates.
Kusajiriwa kwa mchezaji huyu katika klabu ya Arsenal kuna hitimisha lile Dukuduku kwa mashabiki kutaka wachezaji wa kiwango cha kimataifa ambacho walikuwa wa kililia kwa muda mrefu , Hasa baada ya kuifunga Tottenham na inaonekana sasa kuwa hakutakuwa na shaka tena kwa klabu hiyo na wataakuwa washindani wa kweli katika ligi kuu ya uingereza na sio kama ilivyokuwa mwanzo kushabikia nafasi ya nne.
Mjerumani huyu ana aamini kuliko wanavyoamini wengine .kwa kusaini Arsenal, Anasema: ‘Nina Tazama Mbele katika maisha yangu mapya nikiwa na arsenal.
‘Niliishi vizuri katika miaka yangu mitatu pale Real Madrid, Sehemu amabayo nimeweza kubadilika na kuendelea kiakiri na kibinafsi .
‘Tumeshinda makombe matatu ,Lakini sasa natazama maisha mapya nikiwa na Arsenal.
Marouane Fellaini’s anatimiza ndoto ya kuungana mkufunzi wake wa zamani kule Manchester United baada ya kuungana na David Moyes na alikuwa katika mizani ya kati hadi uhamisho wake ulipo kamilika .
Everton na United hawakuelewana mpaka walipokuja kuafikia kuwa walipane kiasi cha Pauni £27.5million.
Fellaini anatakiwa Kumshukuru James McCarthy . Kwani kiungo huyo amesaini Dili ya Pauni £13million kuelekea Goodison Park kuungana tena na Roberto Martinez Kabla Dirisha kufungwa ,huku mchezaji akiziiba nafasi ya iliyoachwa wazi na Fellaini.
Mpaka sasa bado hakijaeleweka kuhusu mchezaji kama uhamisho umekamailka ama bado lakini litafahamia tu pale wakuu wa maswala ya uhamisho watakapo kaa chini na kulifanyia utafiti swala hili ,Ni mlinzi wa Kushoto wa Real Madrid Fabio Coentrao amabaye ameripotiwa akienda kwenda Old Trafford kwa Mkopo wa Muda Mrefu.
Lakini halikuwa jambo la siri Moyes alikuwa akimuhitaji mlinzi wa kushoto wa Everton Leighton Baines,lakini hakuna mshabiki ambaye atakubali tuhuma za Coentrao.
Japokuwa ,Hata saa za Asubuhi Ya Leo bado hakuja fahamika,Lakini kuna majadiliano yanaendelea kama uhamisho ulifanyika kwa wakati ama sivyo .
Maafisa wa La Liga wanathibitisha Taarifa kabla, ilishatangazwa pia kukamilika kwa uhamisho wa Mkopo wa wa muda mrefu wa mchezaji wa Granada Guilherme Siqueira - ili waeze kumruhusu Coentrao’s kuondoka .
Siqueria aliishia kujiunga na Benfica,Huku dili ya Coentrao’s ikiwa ina ning'inia ,maafisa wa wakiwa wanaitazama taarifa yao ya mwanzzo .
.
11.30... Romelu Lukaku Anasaini Everton
Hii ilikuwa na Maana ya kuwa msimu huu utakuwa wa Lukaku’s . Baada ya kuonekana kuwa kijana huyu Anarejea Chelsea baada ya Kwenda kwa Mkopo wa Muda mrefu kule West Brom, wengi waliona kuwa kijana huyu kutoka Belgie angeweza kutengeneza timu nzuri zaidi .
Japokuwa ,Majuma kadhaa katika msimu mpya , Lukaku amecheza mechi Tatu tu na zote akitokea kwenye Benchi na ya mwisho ilikuwa ya Super Cup,Na kwa bahati mbaya kuishia kukosa mkwaju wa pernaty kuifanya Bayern Munich kutwaa ubingwa - na sasa amekwenda Goodison Park kwa mkopo wa Muda Mrefu .
No comments:
Post a Comment