Klabu ya soka yanga ya Dar Es salaam
leo imeonyesha leseni inayomruhusu
mchezaji wake mpya Emanuel Arnod Okwi
kuchezea klabu hiyo katika michuano ya kimataifa baada ya kutokea mikanganyiko
ya muda mrefu kwa kutokuelewana baina ya wadau wa soka mawakala ,vyombo vya habari,
fifa na shirkisho la soka afrika caf na klabu ya Etoile du Sahel .
Msemaji wa klabu ya yanga Baraka
kizuguto ameonyesha leseni hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhsu maandalizi ya timu hiyo dhidi ya timu soka ya Al AHLY katika michuano ya klabu bingwa barani afrika
mchezo utakao chezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa taifa jiji Dar Es
salaam mzunguko wa pili kuwani ubingwa wa afrika ambapo al ahly ni Bingwa
mtetezi.
Emanuel alikuwa akiitumia klabu ya
simba kabla ya kuuzwa kwenda katika klabu ya Etoile Du sahel ya Tunisia ambapo mapaka leo simba haija pata pesa zake
katika hari ambayo bado haijafamika mpaka leo haijajulikana kama kandarasi ya
mchezaji huyo imekwisha au bado lakini kulilipotiwa kuwa aliwahi kuishtaki
klabu hiyo kuwa haijampatia mshahara wa miezi mitatu na hivyo kuvunjika rasmi
mkataba wake nahii ni kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo na Emanuel okwi
mwenyewe.
Lakini kwa upande mwingine Klabu ya
sahel ilimshtaki Okwi fifa kuwa ni mtoro baada ya kushindwa kurudi katika klabu
ya sahel wakati alipokwenda kuitumkia timu ya taifa ya uganda katika mmichano ya kombe la dunia , kitendo kinachosemekana mpaka leo hakijafanyika kwa okwi.
Lakini shirikisho la soka la kandanda
la Tanzania liliwahi kuuliza kuhusu mustakbari wa mchezaji huyo kuchezea klabu
ya Yanga na kwa mujibu wa barau hiyo ilisema hivi “Jukumu la kumuidhinisha
mchezaji kucheza katika timu ya nchi husika ni jukumu la chama cha soka cha
nchi husika na kama mmefuata sheria inavyotakiwa haina tatizo “
Lakini katika hari isikuwa ya
kutegemewa Mwenyekiti wa klabu ya soka ya simba
alikuwa na nyaraka za siri za ambazo anadai alitumiwa na Sahel ya Tunisia zikionyesha kuwa Okwii ni
mali ya sahel .
Lakini je nini kitatokea katika
sinema hii ya sakata la Emanuel okwi ambalo Etoile Du sahel na Shirkisho la soka
Afrika Caf ambao ndio wametoa leseni huku Al AHLY wakionekana kanakwamba hawajui kinachoendelea
ni jambo la kusubiri kisheria kwani zipo mechi nyingi ambazo matokea yamewahi
kutenguliwa kutokana blanda za kuchezesha wachezaji isivyo utaratibu.
No comments:
Post a Comment