Shirikisho la mpira wa miguu la Tanzania tff limevunja mkataba na
aliyekuwa mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania Kim Poulsen ,Rais wa tff Jamal Malinzi amesema kuwa
wamekubaliana kuvunja mkataba kwa makubaliano
maalum na ni siri kati ya Shirikisho na
kocha lakini amesema serikali inatambua kuhusu hari hiyo.
Licha kubanwa na maswali ya waandishi
wa habari rais wa tff bado hakutaka kuweka hadharani ni kiasi gani kimeigharimu
Tanzania kulipa pesa za kuvunja kandarasi hiyo ambayo ilibidi imalizike 2015
kwa upande mwingine inaonekana wazi kuwa kocha anayekuja kuifundisha Tanzania anaweza
kutokea uholanzi kwani baada ya kubanwa na waandishi wa habari ataje angalau
nchi anayotoka kocha anayekuja alitaja nchi ambazo ujerumani ambayo ina kocha
mmoja na uholanzi makocha wawili ambao wamebakia katika mchujo unaoendeshwa na
chama hicho.
Aidha kwa upande wake Kim alionekana
kutoa Tathmini ya mafanikio aliyoyapata
tangu alipoteuliwa kuifundisha stars huku akionekana kutetea CV yake lakini akaweka
wazi kuwa wachezaji wa kitanzania ni wafupi na wavivu wa kula ndio maana
walipocheza na Ivory coast iliwapa sana tabu na matokeo yake wakapoteza mchezo
lakini ameipongeza Ivory coast kuwa ni timu nzuri na inastahiri kucheza kombe la
Dunia.
Na yeye alipoulizwa kuhusu gharama ya
kuvunja kandarasi hiyo majibu yalikuwa ni yale yale aliyotoa Rais Malinzi huku
akitilia mkazo kuwa katika ofisi yoyote lazima kuwe na mabadiliko.
No comments:
Post a Comment