Leo natazama jinsi
mashabiki wanavyoweza kuwazidi nguvu viongozi wa soka la Tanzania naama bila
shaka unaanza kusoma kwa hamu sasa nakujiuliza ni nguvu ya aina gani hiyo?
Ninaposema mashabiki
wanawazidi viongozi kimaamuzi ni pale unapotazama ufanyaji kazi wao, Mtu pekee aliyewahi kuja Tanzania na kufundisha
soka marcio maximo , aliyemwka mtu anayedaiwa kuwa mlinda mlango nambari Juma
Kaseja kwa utovu wa nidhamu licha ya kupigiwa makelele na mashabiki wa soka
Marcio hakubadirisha msimamo kiasi cha kuchukiwa na baadhi ya mashabiki wa timu
aliyokuwa akichezea .
Leo hii wapo baadhi
ya viongozi wa kitanzania ambao wameshindwa kusimama kidete kufumba macho na kutupilia mbali kile
ambacho mashabiki wa soaka wanataka ,
katika soka la Tanzania mashabiki wananguvu kubwa sana na ukiwafwatisha
wanaweza kukupoteza kabisa kwani hata kama wazo walitoa wao ukifungwa
watakubadilikia tu watasahau kama wao ndio walio kushauri.
Yapo mambo ambayo
yameshafanywa katika shirikisho la soka la Tanzania kama kuanzisha mfumo wa
Muda mfupi kama anavyoita Rais wa tff Jamali malinzi sina maana ya kutofautiana
kimaamuzi bali ninantofautiana nae kimawazo kwani unaweza kuamua bila kufikiria
wakati mwingine.
Sioni haja yakuwa na
haja mchakato wa muida mfupi kwani kama timu ya taifa ya Tanzania ipo young
taifa stars ipo kuna haja gani ya
kutafuta wachezaji kutoka kila eneo la Tanzania hii leo kwa kutumia maimilioni ya shiringi kwani wale
vijana wa miaka yote ya Copa coca cola wamekwenda wapi nia ya malinzi imekuwa kutaka kuleta timu ya
taifa yenye sura ya muungano binafsi yangu nina jaribu kutazama ni lini timu ya
taifa imeshindwa kuwa na sura ya muungano au ni hoja za kisiasa za kutaka watu
wa Zanzibar wamuone kuwa wamepata mtu anayewajari sana .
Pengine malinzi hajui
pengine hajawahi kukaa na wazanzibar
mimi ninamsaidia leo hii Wazanzibar wanachotaka sio hicho wnataka Uanachama Fifa
sio kingine hawana mpango wa kutaka timu ya taifa ya pamoja kila mwaka wamekuwa
wakiona wachezaji wao wakicheza katika timu ya taifa ya Tanzania lakini sio
wengi kiasi hicho .
Hapa ndipo ninaposema
kuwa anazidiwa na maamuzi na washabaiki viongozi wanakwenda kutokana na nguvu
ya mashabiki .sio nguvu zao za Binafsi viongozi wengi wa soka la Tanzania
wanatazama upepo wa mashabiki wanataka nini mechi zinapochezwa kiwanjani mabo
mengi hufanywa kutoka na nguvu ya mashabiki majukwaani je? Unafikiri
tutafika .
Mwaka elfu mbili na
mbili rais wa Brazil Da Silva aliwahi kumwambia Luis felipe Scolari kama hatomjumuisha Romario De souza na
kutokuchukua ubingwa basi asirudi Brazil
lakini Big Phil alishikiria msimamo wake na kumwacha De souza na wakachukua
ubingwa.
Lakini kwa Tanzania viongozi
wengi wanashindwa na nguvu na mashabiki
na kufanya kazi kwa upepo wa mashabiki ukikaa jukwaani na kusikiliza
mashabiki wao tayari ni makocha kabla ya kuwa makocha .
Je kuna
haja ya kwenda kushiriki michuano ya mataifa ya afrika tu kwanini tusiwe na
lengo la kujenga mifumo ya soka kwanza shida iliyopo kila mmoja katika uongozi
anataka kufanya jambo nili akumbukwe kuwa alitufikisha mahala fulani wakati
mwingine hizo huwa sifa za ambazo
haziwasaidii watanzania .
No comments:
Post a Comment