SIKIZA SAUTI HAPA
Leo hii nimepita
katika shule ambayo nilisoma kuanzia Darasa la kwanza mpaka la Saba shule ya msingi Mtakuja shule ambayo imenikuza, nilikwenda
kutembelea kutazama sera ya michezo
inavyotekelezwa shuleni hapo kwa hakika ukifika tu shuleni hapakupi hamu ya kufikiri kuwa kuna harakati zozote za
michezo katika shule hii na hapo ndipo unapoona kuwa ndoto za Tanzania kushiriki
michuano mikubwa ya kimataifa hasa ya vijana .
Ni kweli kabisa
unavyoona hapo pichani sidhani kama kuna mzazi ambaye anataka kumpeleka mwanafunzi
katika shule kama hiii walio wengi wanaopeleka watoto wao hapa uwezo wao ni wa
chini sana katika kipato chao cha kifedha na ni wanafunzi wachache sana ambao
hufanikiwa kusonga mbele zaidi hata kielimu.
Ni jambo la kawaida
sana kusikia katika vyombo vya habari kuwa michezo inapigiwa upatu kuwa
imerejeshwa lakini ukitazama sio kwa asilimia mia moja kwa sababu kama kipindi
cha michezo hakuna sio rahisi kwa wanafunzi kama hawa kuweza kuelewa nini
kinachoendelea katika ulimwengu wa michezo
kwa hakika wanafunzi wengi wanawajua wachezaji wa kimataifa nyakati nyingine unaweza kushangaa wanayajua vipi.
Lakini kama
mwanafunzi anaweza kunasa mchezo mzima wa mpira wa miguu ambao unaooneshwa katika
televisheni na kukuelezea kila kitu ni rahisi sana kama angepata mafunzo ya
kipindi cha michezo kikafundishwa kuhusu kwa ujumla na mchezo aupendao kwa
dakika japo thelathini kila mwisho wa wiki lakini bado jambo hili hakuna katika
hari ilivyosasa ni vigumu sana kuinua michezo Tanzania
Nimefanya mazungumzo
na Na mwalimu wa michezo katika shule ya msingi Mtakuja aliyejitambulisha kwa
jina moja tu la Chirwa ambaye yeye binafsi na mwenyeji wa Ruvuma
No comments:
Post a Comment