Wachezaji 31 wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa
ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya michuano
ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Senegal.
BOFYA HAPA
Ngorongoro Heroes itakayokuwa chini ya Kaimu Kocha
John Simkoko akisaidiwa na Mohamed Ayoub inaingia kambini kesho (Machi 19 mwaka
huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza dhidi ya Kenya
itakayochezwa kati ya Aprili 4-6 jijini Nairobi.
Kikosi kinachounda timu hiyo ambayo itarudiana na
Kenya kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinajumuisha pia
baadhi ya wachezaji walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili
ya maboresho ya Taifa Stars.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam),
Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke), Manyika Peter Manyika (Scouting- Ilala) na
Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende, Zanzibar).
Mabeki wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union),
Edward Charles (JKT Ruvu), Frank Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel
Gadiel Michael (Azam), Hussein Mkongo (Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed
(Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki
Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani (Majimaji).
Viungo ni Ally Nassoro (Coastal Union), Bryson
Raphael (Azam), Farid Musa (Azam), Hamid Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande
(Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti
United), Mohamed Issa Juma (Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin
(Scouting- Kinondoni), Seleman Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John
(Scouting- Mwanza).
Washambuliaji ni Ally Salum Kabunda (Ashanti
United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto, Zanzibar), Jafari Mwambusi (Mbeya
City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal (Mlale JKT), Salum Abdilah Mineli
(Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania Prisons).
No comments:
Post a Comment