Makundi ya
Kombe la Dunia yamepangwa Nchini Brazil siku ya ijumaa huku matarajio ya
waafrika wakitamani Baadhi ya timu zao kutokukumbana na Timu ngumu zaidi ambazo
zinajulikana kidunia Kwa mtazamo wa Mashabiki wengi wa soka la afrika kuwa ni
hatari zaidi .
Kundi A ambalo linatimu za Brazil, Croatia, Mexico, Cameroon ukilitizama kundi hili sio jepesi wa gumu kwa
timu ya afrika unapocheza kombe la dunia lazima ufanye kazi ya ziada kwani
katika kumbukmbu zangu hakuna timu iliyotwaa ubingwa wa dunia bila kuifunga
timu kigogo hii inaonyesha wazi kuwa afrika tuwaoga sana katika mashindano hasa
ya kombe la dunia Wanachotakiwa kukifanya Cameroun ni kujipanga na kutafakari
katika kucheza kimahesabu tu na kuwa mechi iliyopo mbele yako na sio ambayo
haujacheza siku zote afrika huwa tunahisi kuonewa au kupangwa makundi magumu
kitu ambacho sio kweli kwani mara zote timu hupangwa kutokana na Viwango vya fifa
ukiwazatazama wachezaji waafrika wanaocheza ulaya ukutana na wachezaji
wanaocheza vilabu hivyo hivyo iweje muwe waoga tunahitaji kujiamni na kufanikisha
azma ya kuwa hakuna kisichowezekana ili uchukue ubingwa dunia lazima ufe.
Kundi C: Colombia, Greece,
Côte d’Ivoire, Japan Timu
ya ivory coast ambayo imekuwa ikiomba kila mwaka kuwa isikutane na timu vigogo kwa
mtazamo wao wanaweza kufurahi lakini mimi sioni cha kufurahia kwani ukitazama
timu walizopangwa nazo ndizo hatari zaidi Colombia inacheza soka kama la Brazil
,Ugiriki hawa ndio waliwahi kumtoa kamasi Cristiano Ronaldo na ureno yake katika
fainali za ulaya mwaka 2004 Japana ni timu amabayo inashiriki kombe la dunia
kwa takriban mara ya saba ukilinganisha na Ivory coast mara ya pili kwa hiyo
inakuatana na timu zenye uzoefu je unafikiri ni kazi rahisi hapana la hasha
kazi ni ngumu sana hakuna mchekea kwa timu za afrika zinazotaka urahisi kwani
sijui ni nani aliwaambia kombe la dunia ni rahisi wanachaotakiwa kukifanya
ndugiu zangu hawa afrika ni kujipanga na kumsikiliza mkufunzi anasema nini
na wao ndicho wanachotakiwa kukifuata kiwanjani.
Kundi F : Argentina, Bosnia-Herzegovina,
Iran, Nigeria
wawa kilishi wa afrika Nigeria na Mabingwa wa afrika wanakutana tena na
Argentina timu walioishinda katika fainali za kombe la Olimpik mwaka 1996 kule
Atlanta Marekani wakakutana tena Korea /japan sasa kuna haja gani ya kuiogopa
Argentina timu waliyowahi kuifunga fainali najua wanaweza kuzidharau Nchi kama
Iran,na Bosnia-Herzegovina na hapo ndipo watakapofungwa kwani wenzao hawadharau
timu wanazokutananazo mara nyimngi timu za afrika huwa zinafungwa katika
fainali za kombe la dunia kwa kudharau maadui zao kugombania posho kutoka
katika vyama vyao huku wakishindwa kucheza mechi zao wakati fifa inawapa pesa zaidi ya wanazogomea
huu ndio ujinga wa afrika.
G: Germany, Portugal, Ghana, USA hata
katika kundi hili sioni kama kuna tatizo Ghana ilishacheza na Ujerumani mwaka
2010 nchi afrika kusini katika fainali za kombe la dunia ilishacheza na
marekani kwa hiyo inazijua Nje ndani timu inazocheza nazo hakuna haja ya kubabaika ni kujipanga unapogopa na kuanza kusema kundi gumu hivi hata
kama utapewa kundi ujipangie mwenyewe bado utafungwa . kauli yangu ni ile ile
tuingie kiwanjani tucheze hakuna jambo jepesi katika dunia hii .
Belgium, Algeria, Russia, Korea Republic
nina maliza kwa wawakilishi pekee kutoka katika kanda ya afrika kaskazini nawao
wanatakiwa kufanya yale ambayo nimeayaandika kwani kama mpira ni ule ule
viwanja ni vile vile huwa nasema siku zote hakuna jambo la hisi swala la msingi
ni kushika yale ambayo mwalimu anasema katika vyumba vya kubadilishia na kuachana
na dhana ya kusema tunapangiwa makundi magumu kwani hakuna siku tutapangiwa
kundi jespesi hata siku moja kwa hiyo rai yangu kuwa timu za afrika kuwa
tumeshajua timu tunacheza nazo la msingi ni kutamaza namna zinavyocheza na
namna zinavyofundishwa na aina ya mpira wanaocheza tufikirie mechi iliyopo
mbele yetu na sio tutakuatana na nani mechi ijayo .
No comments:
Post a Comment