Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini
Tanga.
Shughuli
inayoendelea kwa sasa ni kupima udongo (soil test) na kuandaa michoro kwa ajili
ya ujenzi wa kituo cha michezo (Sports Complex) ukiwemo uwanja wa mpira wa
miguu na majukwaa yake.
TFF
imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la kujenga
kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa yake.
Pia
Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara waliovamia
uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial ground) mjini Moshi.
TFF
inawakumbusha viongozi wa vyama vya mikoa ambao hawajaomba maeneo ya kujenga
vituo vya michezo vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu, waongeze jitihada za kufanya
hivyo, TFF itawaunga mkono.
TFF
inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama tayari
vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na kuendeleza maeneo
kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu.
TFF
inaahidi kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu
haitasita kufanya hivyo.
Wakati
huo huo, TFF inalishukuru Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa
kukubali kugharamia uwekaji nyasi za bandia kwenye Uwanja wa Kaitaba, na pia kusaidia
uendelezaji wa uwanja wa TFF wa Tanga.
No comments:
Post a Comment