Katika hari isiyo yakawaida
unapokuwa katika uwanja wa taifa Goli linapofungwa au kukoswa utaskia kelele
nyingi za furaha au kwa mashabiki ambao ni zaidi ya Elfu arobaini katika uwanja
wa taifa lakini je hawa wanaoshangilia wanaelewa wanachoshangilia kwani mara
kadhaa hutokea kufungwa magoli ya ambayo hata kipofu hawezi kukosa na mtu
anayekosa ni mtu ambaye anaaminika sana katika timu au kufanya Madhambi ambao
pengine huwezi kuamini .
Ugaidi wa soka la Tanzania upo
katika maeneo mengine na yapo mambo yanayofanyika Ndani ya kiwanja na nje ya
kiwanja lakini kikubwa ambacho watu wanatakiwa kuelewa ni kuwa yanayofwanya nje
ya uwanja yanaathari kubwa zaidi ambayo Mashabiki wengi wanaokaa majukwaani
hawajui maskini ya Mungu nini kinaendelea
ndani ya kiwanja na laiti wangejua sidhani kama wangekuwa wanakwenda
kiwanjani kutazama huo mpira wenyewe.
jambo la kwanza kwanini simba na yanga
zimekuwa zikigombana sana zenyewe kwa zenyewe kuhusu wachezaji katika hasa
wakati wa usajiri na kujaa fitna nyingi sana ,na mwisho wa siku Eidha kuishia
kutocheza kabisa mpira wenyewe lakini yafuatayo yanaweza kusababisha hari hiyo,
Upangaji wa matokeo uliokithiri,uchawi,mapenzi ya timu unayoshabikia haya ni mambo yanaisibu soka Tanzania.
Kwa ulaya sio rahisi na
ukigundulika Ni hatari sana unawezafungiwa maisha yako yote kujihusisha na soka
kabisa kwa Tanzania Mchezaji anaweza kuwa Mwanachama wa simba na akawa anacheza
yanga na kwa hari ya kitanzania mambo haya ni magumu sana wewe msomaji wa
kawaida kuyaamini lakini nina kuhakikishia ya kuwa Mechi nyingi za ligi kuu ya
Tanzania kwa asilimia 70 Matokeo yanaweza julikana kabla hata ya mechi kuchezwa.
na hii ni kwa miaka mingi imetokea na
tatizo hili alijaanza leo ni kwa muda mrefu sasa mambo haya yanafanyika
japokuwa kunaweza kusiwe na ushahidi wa kutosha wa hari hii.
Ni kwa hari hii mamilioni ya
watanzania huzungumza soka kwa undani pasipo kujua nini kinaendelea hasa
mashabiki wa wanaosoma magazeti na kukaa vijiweni na wengine wakithubutu
kuwafananisha wachezaji wao na wachezaji nguli wa kimataifa labda kabla
sijaenda mbali nikupe nukuu hii ya Mchezaji mmoja aliyetoka klabu moja kubwa na
kwenda klabu nyingine kubwa.
Mfano Mchezaji anaweza sema hivi “Mimi
mpira ni kazi yangu kama Simba wakihitaji msaada kwangu nitawasaidia na kwenda
Yanga kucheza mpira” Je kauli hii unaeielewa waje msomaji wangu? .
Soka ya Tanzania ina usaliti wa hari ya juu
mnawezaje kufanya mazoezi kiwanjani kwa uaminifu na kujipinda lakini kwenye
mechi anapitwa kirahisi kabisa pasi na hata kujishuhurisha hata Chembe je haya ninayokueleza huoni kama ni usaliti
ulio kithiri mashabiki hawajui kamati za ufundi na wanachama na viongozi na
kama za utendaji zina kazi gani asilimia kubwa ya wachezaji wote wanaocheza
katika timu za ligi kuu Bara ni Simba na yanga kiushabiki na wengine wanachama
wa klabu hizo .
Sasa huoni kama kuna usaliti hapo
unaweza kuona kama natania katika kueleza mambo hayo kwa muda mrefu
Bingwa wa Ligi ya Tanzania sio halisi, na kuna fitna za hari ya juu lakini
maskini ya Mungu mashabiki wa hari ya juu huwa hawaelewi nini kinaendelea ndani
na nje ya kiwanja.
Usaliti upo kwa wachezaji na
Viongozi na maskini ya Mungu makocha wa Kigeni na huwa hawajui hujikuta
wakistaajabu matokeo ya uwanja bila kujua kinachoendelea hii ina maana kuwa soka Huchezwa kabla ya kuchezwa.
No comments:
Post a Comment