Manchester United imechemka kutinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kufungwa na Bayern Munich huku wakiendeleza ushindi katika katika Record baina yao .
United inayoongozwa na David Moyes's ilitoka suluhu na Bayern ya 1-1 katika Dimba la Old Trafford katika mzunguko wa kwanza na walianza vizuri baada ya Patrice Evra kufunga la uongozi japo bao hilo lililudumu kwa dakika moja katika kipindi cha pili.
Baada ya Mario Mandzukic kusawazisha bao hilo kwa kichwa na kabla ya Thomas Muller's ajamalizia krosi iliyopigwa na Ribery kupachika bao la pili .
Alikuwa Arjen Robben tena aliyekata chenga na kupiga shuti lilimparaza Vidic na kumpoteza maboya De gea na kufuga bao la tatu na matokeo kusomeka 4-2 kwa jumla .
Atletico Madrid imeitoa Barcelona katika ligi ya mabingwa baada ya
Koke kufunga goli la mapaema katika mzunguko wa pili katika dimba la Vicente
Calderon.
Kichwa kilichopigwa na kiungo huyo na kuipa timu yake uongozi wa goli mbili moja kwa ushindi wa jumla .
Madrid walipiga mashuti matatu ndani ya dakika ishirini.
Gabi alipoteza nafasi ambayo ingemfanya kumaliza mechi mapema , Huku Neymar akijaribu kusawazisha na kwa kuruka kichwa cha kuchupa kwa chini lakini haikusaidia .
No comments:
Post a Comment