Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubaliana na uamuzi uliofanywa na Kamati
ya Maadili katika malalamiko mawili ambayo iliyawasilisha mbele yake, hivyo
haitakata rufani.
Katibu
Mkuu wa TFF aliwasilisha mashauri mawili mbele ya Kamati hiyo iliyoongozwa na
William Erio. Malalamiko ya kwanza yalikuwa dhidi ya waamuzi wenye beji za
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga na Samwel Mpenzu na wakufunzi wa waamuzi Riziki Majala na Mchungaji
Army Sentimea.
Wote aliwalalamikia kwa kuwafanyisha mitihani
(wakufunzi), na waamuzi kufanya mitihani hiyo kinyume na utaratibu pamoja na
kughushi matokeo.
Kamati katika uamuzi wake iliiagiza waamuzi hao
kufanya upya mtihani huo katika robo inayofuata ambapo wakifaulu waendelee
kuchezesha mechi. Waamuzi wa FIFA hufanya mitihani hiyo mara nne kwa mwaka.
Kwa upande wa shauri dhidi ya Ofisa Takwimu wa TFF,
Sabri Mtulla ambaye alilalamikiwa kwa kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi dhidi ya mchezaji Emmanuel Okwi, Kamati
iliagiza suala hilo liwasilishwe upya pamoja na ushahidi wa kuthibitisha
malalamiko hayo.
No comments:
Post a Comment