Atletico Madrid imepata ushindi na kulipiza kisasi cha kufungwa na Real Madrid katika ligi ya Mabingwa ulaya baada ya kuwafunga katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu .
Mabingwa watetezi wa La Liga Atletico walipata Goli la kuongoza katika Dimba la Bernabeu wakati Tiago alipofunga kwa kichwa kwa mpira wa kona .
Cristiano Ronaldo,alifunga goli la kusawazisha akitokea kwenye majeruhi kwa penati , na kuifanya Madrid kusawazisha .
lakini Atletico, ambao walijitahidi kukabiliana na kelele za mshabiki wa Real , walishinda mechi hiyo kwa goli lililofungwa na Arda Turan's .
No comments:
Post a Comment