Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya
Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (SAFA) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na
kipa wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Senzo Meyiwa.
Ametuma salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na
Rais wa SAFA, Danny Jordan na kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za
vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki
hii.
Rais Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa
Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na
mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu.
Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu
zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa
na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito
kwao.
Rais Sata (77) alifariki dunia juzi kwenye Hospitali
ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa
Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mjini Vosloorus.
No comments:
Post a Comment