28 August 2012

KAMATI YA SHERIA KUPITIA USAJILI SEPT 2

Alex Mgongolwa Mwenyekiti wa kamati ya sheria Tff




Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2012/2013.
  Usajili utakaopitiwa ni wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Lidi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo Kamati itapitia pingamizi zilizowasilishwa na klabu mbalimbali dhidi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu zingine.Taarifa hiyo imetolewa na afisa habari wa shirkisho la mpira wa miguu tanzania tff Boniface wambura.

No comments:

Post a Comment