HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

29 August 2012

KENYA YAIPA NAFASI SERENGETI KUIVAA MISRI




Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) sasa itaivaa Misri kwenye raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 10 za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
 
Awali Serengeti Boys ilikuwa icheze raundi ya kwanza dhidi ya Kenya, mechi ya kwanza ikichezwa Septemba 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) jana lilituma taarifa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likielezea kujitoa kwenye michuano hiyo.
 
Serengeti Boys itaanzia nyumbani Oktoba 14 mwaka huu, wakati ya marudiano itachezwa nchini Misri kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu. Mshindi baada ya mechi hizo mbili ataingia raundi ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho kabla ya kwenda Morocco.
 
Katika raundi ya tatu ambayo mechi zake zitachezwa katikati ya Novemba na ya marudiano mwisho mwa mwezi huo, mshindi kati ya Tanzania/Misri atacheza na mshindi wa mechi ya Congo Brazzaville dhidi ya Msumbiji/Zimbabwe ambazo zinapambana katika raundi ya kwanza

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers