HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

30 August 2012

MBUYU ATUA DAR LEO HII ALAKIWA NA MAMIA YA MASHABIKI WA YANGA



Aliyevalia jezi nambari nne ni mchezaji mpya wa dar es salaam yanga afrika Mbuyu Twite akiwa ameveshwa jezi namba 4 ikiwa imeandikwa kwa Dhihaka jina moja la mwenyekiti wa klabu ya simba ya jijini DSM


  Mlinzi mpya wa klabu ya soka  Yanga, Mbuyu Twite amewasiri leo jijini Dar es salaam na kulakiwa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo katika uwanja wa Ndege wa JKN  ambapo baadaye alipakiwa kwenye gari maalum kulekea makao makuu ya klabu hiyo  mtaa wa Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Aidha hakukuwa na kiongozi yeyote au mashabiki  wa Simba wala askari aliyejaribu kumkamata  kama ilivyokuwa  kumetolewa  Taarifa  la kutaka kumkamata mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda, ambaye ana asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa wangemkata  kwa tuhuma za kujipatia fedha kinyume na utaratibu dola za Kimarekani 30,000, kabla ya kusaini Yanga, Twite alikuwa akitumikia klabu ya APR ya Rwanda alisaini Simba na kuchukua dola 30,000.
, baadaye mchezaji huyo alibadili maamuzi  na kutia saini kandarasi ya  kuhudumu klabu ya  Yanga na kurudisha fedha za Simba kupitia viongozi wa APR na St Eloi Lupopo ya DRC, timu hizo  zilikuwa zinammiliki mchezaji huyo kwa pamoja.
Twite aliianza kuichezea Yanga wiki iliyopita ilipokuwa Kigali, Rwanda kwa ziara ya wiki moja lakini alishindwa kurejea na wenzake Jumatatu kwa kile kilichoelezwa anakamilisha taratibu za kuhamisha familia yake .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers