HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

16 October 2012

ZAWADI YA FAIR PLAY KWA KLOSE MSEMA KWELI MPENZI WA MUNGU


Mshambuliaji wa timu ya soka ya taifa ya Ujerumani Miroslav Klose ampokea zawadi ya heshima ya kuwa muungwana mchezo ni.
mara baada ya kukubali kuwa goli alilofunga katika ligi kuu ya italia mwezi uliopita lilikuwa la mkono kijana huyo mwenye miaka 34 ambaye amefunga magoli 65 katika mechi 125 alizochezea Timu ya taifa ya ujerumani ,ameshinda zawadi  hiyo baada ya kumuelezea mwamuzi kuwa goli alilofunga katika mechi dhdi ya lazio na Napoli ambapo  alifunga mwishoni mwa mwezi september alilifunga kwa mkono 

Baada ya yeye mwenyewe kukiri mwamuzi alifuta goli hilo ambapo lazio ilifungwa mabao matatu kwa sifuri mjerumani huyo alisifiwa na timu pinzani hadi vyombo vya habari vya italia vilimsifu kwa uaminifu wake .
Mwamuzi aliniuliza kama mpira uligusa mkono wangu alisema klose ambaye atakuwemo katika kikosi cha ujerumani dhidi ya sweden huko  Berlin's Olympic Stadium siku ya Jumanne .
''Nilikubari kuwa lilikuwa ni goli la mkono kwa mimi hilo lilikuwa jambo  la kwaida najua kuna watu wengi wadogo watakaa mbele ya vinasa pcha katika runinga na kusema huu ni  mfano mzuri wa kuigwa. 

Klose  alishinda zawadi kama hiyo 2005 alipokuwa akichezea  Werder Bremen katika ligi ya Bundesliga Dhidi ya  Bielefeld. Baada ya  Bremen kuzawadiwa mkwaju wa  penalty,
Klose alimwambia mwamuzi kuwa mlinda mlango wa  Bielefeld alidaka mpira kwanza kabla hajamgusa yeye na kuangauka chini . mwamuzi alighairisha mkwaju wa pernaty na kufuta kadi ya manjano aliyompatia mlinda mlango huyo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers