HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 December 2012

BBC KUTANGAZA MCHEZAJI BORA J3

Wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC mwaka huu
Mshindi wa tuzo  ambayo hutolewa kila mwaka na shirika la habari la BBC atatangazwa rasmi tarehe 17 mwezi huu.

Wachezaji watano wanawania tuzo hiyo  ni pamoja na Yaya Toure Didier Drogba kutoka Ivory Coast, Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na Naodha wa Zambia Christopher Katongo.

Wachezaji hao watano wameonyesha uwezo mkubwa   mwaka huu na wanne kati yao waliongoza vilabu vyao kushinda mataji mbali mbali.

Drogba alihitimisha kandarasi yake na klabu ya Chelsea kwa kufunga goli  la ushindi lililoipa Chelsea ushindi katika fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya, kwa mara ya kwanza na pia kufunga goli   lililoisaidia Chelsea kushinda kombe la FA.

Yaya Toure, amekuwa nyota wa Klabu ya Manchester City ambayo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 44, ilinyakuwa kombe la ligi kuuya Premier ya England.


Nchini Morocco, Belhanda aliongoza klabu yake kushinda kombe la ligi kuu na alifunga magoli 12 na klabu yake ya Montepilla, ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Ufaransa.

Barani Afrika, Chris Katongo aliongoza timu ya taifa ya soka ya Zambia kushinda kombe la mataifa bingwa barani Afrika. Vijana hao wa Chipolopo waliishinda timu ya taifa ya Ivory Coast kwenye fainali hizo.Kinyume na, Katongo, Demba Ba, hakuwa na la kujivunia, katika fainali hizo za Afrika, baada ya Senegal kuondolewa kwenye hatua  ya makundi, lakini akiwa na klabu yake ya Newcastle, Ba, alimaliza ligi akiwa mfungaji bora katika klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tano kwa kufunga magoli 17
Kwa Ujumla wachezaji kumi na mmoja wamewahi kushinda tuzo hili la mchezaji bora wa soka wa BBC.

Jay Jay  Austini Okocha kutoka Nigeria ndiye mchezaji wa pekee ambaye amewahi kushinda Tuzo  hii kwa miaka miwili mfululizo mwaka wa 2003 na 2004.

Miongoni wa walioteuliwa mwaka huu, Drogba amewahi kushinda mara moja naye Yahya Toure hakuwahi kuwa  hata miongoni mwa wachezaji bora watano mwaka uliopita.

Christopher Katongo kwa upande wake atakuwa akiwania kuwa mchezaji wa kwanza kutoka kanda ya  Kusini mwa afrika  kuwahi kushinda tuzo hii.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers