HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 December 2012

Haruna Niyonzima ATIAKANDARASI YA MIAKA MITATU El Merreikh


Mchezaji wa kimataifa wa Amavubi anayechezea klabu ya  Yanga  Haruna Niyonzima anakwenda sudan kwa kandarsi ya miaka mitatu kuchezea  El Merreikh ya sudan .

Nahodha huyo wa  Amavubi ni moja kati ya wachezaji wanaolipwa ujira mkubwa zaidi ambapo imekuwa ikiripotiwa kupokea ujira wa dola za kimarekani   US $3,000  kwa mwezi  bila kujumuisha malupulu  mengine kama gari ya kutembelea  na nakadharika 

Mchezaji huyo wa zamani wa  Etincelles na  Rayon Sport starlet  anaweza kukumbana na kizingiti baada ya klabu yake ya yanga kukataa kuwa haijakaa na kuzungumzia swala hilo la klabu hiyo 

Vyanzo muhimu vya hapa nyumbani vinasema kuwa yanga wameweka dau la dola za kimarekani 
$75,000 )kwa timu itakayomtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda lakini kiwango hicho inaonekana kisilipwe kutokana na mchezaji husika kubakiza miezi sita katika mkataba wake wa sasa   

Haruna alijiunga  na Yanga miaka miwli iliyopita akitokea kwa mabingwa wa ligi ya Rwanda  APR FC kwa uhamisho wa  dollar $30,000 na mshahara wa  USD 1500.
Mchezaji binafsi ameshasema anataka kuondoka yanga 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers