HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

21 December 2012

HATUTADHARAU MECHI "KATONGO "


Christopher Katongo nahodha wa timu ya Taifa ya Zambia akieleza mikakati ya ushindi hapo kesho dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars mchezo utakaopigwa kesho katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Christopher Katongo (30), ambaye pia ni Mwanasoka Bora wa Afrika wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mwaka huu, amesema kuwa mipango endelevu ya kulea wachezaji vijana na nidhamu ya wachezaji ndiyo chanzo cha mafanikio yao.

 Amesema kwamba hata katika mechi ya timu yake dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi, wachezaji wenye umri mdogo ndiwo watakaopewa kipaumbele katika kikosi cha Chipolopolo.

 “Nidhamu, kujituma na kufuata taratibu ndiyo siri ya mafanikio yetu. Nadhani umeona mazoezi yetu, tunafanya kazi kwa umoja na kila mchezaji ana ari ya kufanya kile anachoelekezwa na mwalimu,” .

Kocha wa kikosi wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars Kim Poulsen alikielezea namna atakavyotumia nafasi ya kesho ya kucheza na timu bora ya Afrika Zambi hapo kesho, ambapo ameeleza kuwa anamatumaini ya kushinda katika mchezo huo licha ya kuwakosa wachezaji wake wawili muhimu Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.
 “

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers