HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

23 July 2014

FIFA YATEGWA NA NDEGE YA MALAYSIA BAADA YA KUTUNGULIWA KATIKA ANGA UKRANE

 Angela Merkel

Baadhi ya wanasiasa wakubwa Nchini Ujerumani akiwemo Kiongozi wa Nchi hiyo  Angela Merkel’ ambaye anaongoza chama   kisichopenda mabadiliko  ameongeza joto la kutaka kupokwa kwa Urusi kunyang'anywa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwaka 2018 baada ya kutunguliwa kwa Ndege ya Malaysia iliyokuwa ikipita katika Anga la  Ukrane.
Nchi za Magharibi wamekilaum kikundi kinachosadika kuwa kinatoka urusi katika kupinga jimbo la Kiev’s kujitoa mashariki mwa Ukraine  Baada ya Kuitungua Ndege ya  Malaysia Airlines  MH17 siku ya Tarehe 17 July Ambapo jumla ya watu  298 waliuawa.
Umoja wa ulaya bado unataka kuweka Vikwazo zaidi vya kiuchumi kwa Nchi ya Hiyo ambapo jana Jumanne mawaziri walichelea kufanya maamuzi na watasubiri kwa siku kadhaa .
Kuipokonya Urusi kuandaa kombe la Dunia itakuwa suluhisho zuri zaidi la kiuchumi kuliko kuiwekea Vikwazo cha Kiuchumi , Alisema  Michael Fuchs, Ambaye ni makamu kiongozi wa chama kisipenda mabaliko Katika Bunge la  Ujerumani .
“Fifa Inatakiwa kufikiria kuhusu  Moscow kama kweli inaweza kuandaa mashindano kwani imeshindwa hata kutoa uhakika wa Anga yake katika usafiri wa Ndege ,” Fuchs ameliamba gazeti moja la  Handelsblatt Online, Amesema Ujerumani na Ufaransa wanaweza kuandaa michuano hii kwa haraka sana .
Vikwazo vya Kiuchumi hawezi kuikaba sana Urusi ukizingatia Urusi ina mipaka mikubwa sana , Ambayo ni migumu sana kulinda Bidhaa mbalimbali  zisiweze kuingizwa nchini humo ,  .

Vyama vya biashara vya Ujrerumani vimesema kuwa  Vikwazo vya Umoja wa Ulaya EU vinaweza kuharibu uchumi kati ya   Russia na Ujerumani  ,Kwani  Ndio Nchi ambazo zinakamata Uchumi mkubwa wa Ulaya .
 
 
Waziri wa mambo ya Ndani katika jimbo la  Hesse amekubarina na kauli ya  Fuchs.
“Kama  [Rais wa Urusi  Vladimir] Putin aonyeshi ushiriakiano kabisa katika jambo kubwa la kutunguliwa kwa Ndege , Michuano ya kombe la Dunia kufanyika Urusi 2018 ni ya kufikirika   ,” Peter Beuth amelimbia Gazet hilo la Ujerumani  la Bild.
Stephan Mayer, Ambaye ni mwanachama wa Chama cha kijamii cha umoja  wakristo wasiotaka mabadiliko(CSU),Amesema kuindoa Urusi kutoandaa michuano ya Kombe la Dunia ni jambo safi kabisa.
 
Chama soka cha Ujerumani  (DFB) hakikuwa Tayari kutoa maoni katika mjadala huo ulioitishwa Bungeni siku ya jumamatano kwa maoni yaliyotolewa na wanasiasa ’ .Ujerumani ndio mabingwa wa Dunia wa michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Nchini Mwaka huu  Brazil.
Ndege hiyo ya  Malaysian ilikuwa ikitoka  Amsterdam Kuelekea  Kuala Lumpur na baadae ikatunguliwa maeneo ya Donetsk, ambapo ni ngome ya kuu ya vikosi vya Urusi Dhidi ya Ukraine .
Ambapo Abiria wengi waliokuwemo kwenye Ndege hiyo walikuwa wakitokea Uholanzi , Chama cha soka cha uholanzi kimesema kuwa ni mapema sana kujadiri uhalari wa Urusi kuandaa michuano hiyo 2018 .
“Chama soka cha Uholanzi kimesema kuwa kinaelewa kuwa watu wa uholanzi wanaelewa kumbukumbu mbaya ambayo imetokea katika maisha yao ,” .
“Chama hicho kinaamini kuwa sio jambo sahihi kwa sasa kuzungumiza michuano mpaka uchunguzi utakapo kamilika , ”
Chama soka cha Uingereza kimesema Ni mapema sana kuzungumzia uwezekano wa kuondoa michuano hiyo huko Urusi.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers