HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

21 December 2012

Ni Yaya Toure 2012 APY TENA
Kiungo wa Manchester City  YayaToure ametanagazwa tena kuwa mchezaji Bora wa afrika kwa mara ya pili mfululizo  .

 Toure alimshinda raia Mwenzake wa  Ivory Coast na mchezaji wa zamani wa   Chelsea na mshabuliaji shanghai shenhua  Didier Drogba ambaye ameshika nafasi ya pili wakati mchezaji wa zamani wa Arsenal  kiungo wa timu  ya  Barcelona   Alex Song alikamata nafasi ya tatu .Yaya ameshinda tuzo hiyo ya mwaka  2012 baada ya kupigiwa kura na makocha au wakurugenzi wa ufundi wanaotambuliwa na shirikisho la soka bara la afrika CAF .

 Mshambuliaji wa Zamani wa Barcelona  Samuel Eto'o Ndiye ambaye ameshinda mara nyingi zaidi  tuzo hiyo akishinda mara nne .

 Mabingwa wa Afrika  Zambia imechaguliwa kuwa timu bora ya mwaka wakati kocha wa timu hiyo   Herve Renard amechaguliwa kuwa kocha wa mwaka 2012 .

 Toure, ni moja kati ya wachezaji watakao cheza fainali za mataifa ya afrika mwakani nchini afrika kusini akiwa na timu ya taifa ya ivory coast  .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers