HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

18 January 2013

Azam fc yafika salama Nyumbani kwa Kenyata


 Photo: Wachezaji wapya wa kimataifa waliosajiliwa hivi karibuni, Brian Umony, Jockins Atudo na Humphrey Mieno, David Mwantika, Seif Abdallah na Uhuru Selemani wameanza vizuri katika kikosi hicho kwa kutoa mchango mkubwa kipindi hiki cha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

 

Kwa nyakati tofauti wachezaji hao wameweza kumudu nafasi zao vizuri hali iliyomuondoa shaka kocha msaidizi wa kikosi hicho Kali Ongala.

 

Kali ameiambia tovuti hii www.azamfc.co.tzkuwa wamepata mchango mkubwa kutoka kwa wachezaji hao, wameonyesha umahiri wao na uwezo wa kwa kipindi kifupi walichojiunga na timu hiyo.

 

“Tunafura wanafanya visuri, yalikuwa matarajio yetu kupata wachezaji mahiri kama wao, wamefanya vizuri kadri muda unavyokwenda, tunaamini wakikaa Chamazi kwa pamoja watatoa mchango wao zaidi ya hapa” alisema Kali.

 

Kali aliongeza kuwa wachezaji hao mbali na kufanya vizuri uwanjani wapo karibu sana na wachezaji wenzao hali inayowapa ukaribu na kujenga timu moja hata wanapokuwa uwanjani.

 

Azam FC wakati wa dirisha dogo la usajili imesajili wachezaji hao watatu wa kimataifa, mshambuliaji Umony kutoka Uganda, kiungo Mieno na beki Atudo wote kutoka Kenya.

 

Mbali na hao wachezaji wa aliotoka nadni ya nchi ni Uhuru Selemani, David Mwantika na Abdalah Seif.

 Timu ya Azam FC imewasili salama jijini Nairobi nchini Kenya jana usiku tayari kwa kuanza michezo yake wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya ligi kuu ya Tanzania mzunguko wa pili pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
 
Akizungumzia program nzima ya maandalizi kocha wa Azam FC, Stewart Hall amesema timu itacheza mechi tatu za kirafiki na kufanya mzoezi ya siku mbili katika viwanja vya Nyayo na City.
 
Alisema wachezaji wote wamefika salama, timu itaacheza mchezo wake wa kwanza kesho ‘Jumamosi’ saa 3:30 (15:30hrs) dhidi ya A.F.C Leopard, kwenye Uwanja wa Nyayo.
 
Azam FC leo ‘Ijumaa’ jioni itafanya mazoezi yake ya kwanza katika Uwanja wa Nyayo uliopo katikati ya jijini la Nairobi.
 
“Tutacheza michezo mitatu, michezo yetu itahusisha timu zenye viwango vizuri katika ligi ya Kenya ambazo ni A.F.C Leopard, Sofapaka na K.C.B, mechi hizo zitasaidia kuimarisha timu yangu” alisema Stewart.
 
Kocha Stewart alisema watafanya mazoezi na kucheza mechi katika viwanja aina mbili vyenye nyasi za kawaida na zenye nyasi bandia kwa kuwa katika michezo ya ligi viwanja hivyo vinaendana na mazingira ya Tanzania.
 
Azam FC iliyoko nchini hapa bila ya washambuliaji wake John Bocco na Tchetche Kipre na mchezaji Waziri Salum wanaosumbuliwa na majeruhi, siku ya Jumapili itacheza mechi yake ya pili ya kirafiki dhidi ya SOFAPAKA kwenye uwanja huo huo.
 
Baada ya mchezo huo kikosi hicho kitapumzika siku ya Jumatatu Jan 21, 2013 ambapo watatumia siku hiyo kufanya mazoezi katika Uwanja wa City wenye nyasi bandia.
Azam FC itamaliza safari yake ya maandalizi na mechi za kirafiki siku ya Jumanne Jan 22 ambapo watacheza dhidi ya K.C.B kwenye Uwanja wa City mchezo ambao utakamilisha safari hiyo ya siku saba.
 
Wachezaji walioko jijini ni Mwadini Ally, Aishi Manula, Jackson Wandwi, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, Michael Bolou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru Selemani, Brain Umony, Malika Ndeule, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Abdalah Seif, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Contacts
Ass. Manager Jemedari Said
+255 713528790
 
 
Azam FC Program
 
17th Players Arrive
18th Team Training at Nyayo Stadium 4:00 PM
19th Game vs A.F.C Leopard- Nyayo Stadium 3:30PM
20th Azam FC vs SOFAPAKA –Nyayo Stadium 3:30PM
21st Training at City Stadium 4:00 PM
22nd Game vs K.C.B-City Stadium 4:00PM

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers