HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 January 2013

JOGOO LA UTURUKI LABOTOA KANDAMBILI ZA JANGWANI



Young Africans imepoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Denizlispor ya Uturuki kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika viwanja vya Selen football - Kamelya Complex pemebni kidogo ya mji wa Antalya.

Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema zaidi lakini umaliziaji wa washambuliaji Saimon Msuva na Jerson Tegete katika dakika za 7, 15 na 24 uliikosesha mabao y amapema.

Young Africans ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 35, mfungaji akiwa ni Jerson Tegete akimalizia pasi safi iliyopigwa na Saimon Msuva kufuatia migongeo mizuri ya Haruna Niyonzima na Athuman Idd 'Chuji'.

Young Africans ileindelea kutawala mchezo kwa kipindi chote cha kwanza na hadi timu zinakwenda mapumziko Young Africans ilikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Denizlispor ilifanya mabadiliko ya kikosi chake kuanzai mlinda mlango mpaka washambuliaji wake, lakini mabadiliko hayo bado hayakuweza kuisadia kwani umakii wa walinzi Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro, Kelvin Yondani na Juma Abdul ulikuwa kikwazo kwao kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'.

Dakika ya 78 Denizlispor ilijipatia bao lake la kwanzan, baada ya mfungaji kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni ili hali walinzi wa Young Africans na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' wakisubiri kusikia filimbi ya mamuzi kwani mfungaji kabla ya kufunga alikuwa ameunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Huku mpira ukiwakatika dakika za mwisho kabla ya kumalizika, mwamuzi wa mchezo ambaye hakuonekana kuwa makini aliwapatia wenyeji Denizlispor penati dakika ya 88, penati ambayo ilileta utata kutokana na mwamuzi kupishana malekezo na mshika kibendera aliyekuwa ameonyesha kuwa mshabuliaji wa Denizlispor alikuwa amemfanyia madhambi nahodha Nadir Haroub, Denizli walipiga penati hiyo na kujihesabia bao la pili na la ushindi.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1- 2 Denizlispor FC.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers