HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 January 2013

LULU KAPATA DHAMANA RASMI



Kwa mujibu wa walio mahakamani na kama Mwanahabari mwenzangu Angella Michael Msangi alivyoandika kwenye Ukurasa wake, Lulu kapewa masharti haya:

Kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani,
Kuripoti mahakamani kila tarehe moja ya mwezi,
Wafadhili waweke bond ya mil 20

Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.


story from ayo

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers