28 February 2013

Jordan na Dede Ayew WASTAAFU KUCHEZEA BLACKSTARS YA GHANA



Watoto wawili wa kiume wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana  Abedi Pele wamesema hawakufurahishwa na walivyokuwa  wakitendewa na Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Ghana na wameamua kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Ghana  .

Maamuzi hayo ambayo yamechukuliwa na wachezaji hao wawili  Jordan and Dede Ayew ambao wanachezea timu ya  Olympique Marseille tayari wamekwisha wasiliana na Chama cha soka cha Ghana lakini bado chama hicho hakija thibitisha Taarifa hizo  .
Andre ambaye aliachwa kuchezea timu hiyo katika mataifa ya Afrika alisikitsihwa pia na mdogo wake kuachwa kuichezea timu hiyo katika michuano ya kimataifa ya  kombe la Afrika  kuwa hawakuwa na Nidhamu .
Nyota wa Real Madrid  Michael Essien hayuko tayari kujiunga na Ghana wakati  Kevin - Prince Boateng  bado anasubiriwa kurejea kwenye timu ya taifa ya Ghana baada ya kustaafu Mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment