HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

15 March 2013

TSA KULETA NCHI TISA DAR ES SALAAM


 

 Chama cha mchezo wa Tenis Tanzania  (TSA) kinatarajia kuandaa michuano ya kuogelea  kwa Nchi za Afrika mashariki yatakayo fanyika jijini Dar es Salaam.
 ambapo Tarehe ya mashindano itatangazwa hapo  badae ,Mkurugenzi wa ufundi  , Marcelino Ngalioma amethibitisha .
Amesema kuwa TSA imeshatuma baraua za mialiko kwa   Malawi, Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi,  (DRC) na  Mozambique.
Ngalioma ameongeza kwa kusema  TSA bado ipo katika majadiliano na wadhamini ili waweze kujua hata sehemu ambayo mashindano hayo yatafanyika  .
Mkurugenzi huyo wa ufundi amesema kuwa TSA inatumai kuwa mashindano hayo yataongeza ubora wa viwango kwa wachezaji wake .
“Mashindano hayo ni moja kati ya michuano mikubwa zaidi  na inahitaji msaada mkubwa ili kuweza kufanikishwa na tunayaomba makampuni kutuunga mkono ili kufanikisha mashindano hayo
Aidha maesema ukiacha la kuwaomba wadhamini ameongeza kwa kusema watafanya mashindano kwa kuzingatia viwango vya olimpick kwa kuweka mabwawa ya mita  50 na 100 ili kuweza kukidhi viwango vya Olimpik
 Ngalioma amethibitsiha kuwa zaidi ya washiriki  260  wamekwisha kujiandikisha katika mashindano yatakayofanyika kuanzia kesho katika shule ya  Heaven Of Peace Academy (HOPAC) iliyopo maeneo ya Mbuyuni kunduchi  jijini  Dar es Salaam. 
mashindano hayo ya kesho watayatumia kutazama takwimu za taifa za kuogelea
“Tuna waogeleaji wengi  kutoka  Mwanza, Shinyanga, Zanzibar, Morogoro, Arusha na  Dar es Salaam. na wengine ni wa Tanzanian ambao wanaishi  Kenya,” aliongeza . 
Katika mashindano hayo ya mwishoni mwa juma waogeleaji 20 wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Shirikisho la africa kuogelea  (CANA) katika mashindano ya Zone 3 & 4 yatakayo fanyika   Lusaka mwezi ujao  .
“kwa mwaka jana tulishiriki mashindano hayo na tulishinda Nishani nne fedha moja na tatu na shaba
TSA itaandaa mashindano ya taifa mwezi kenda tarehe  7 - 8 jijini  Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers