HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 March 2013

tunawaasa wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha pikipiki kwa muda wa ziada wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato kwa michezo ni ajira.;Mh. Pereira Silima

 3[1] 
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi zawadi kwa Nahodha  wa timu ya makonde Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)  kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke 4[1] 
Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa Nahodha  wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola  baada ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko  mabao 7-6 katika mikwaju ya Pernaty
 
  6[1] 
Timu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6  baada ya kupiagiana mikwaju ya penati na kuibuka washindi
 
Michuano ya mpinga Cup imemalizika rasmi jana baada ya mchezo wa fainali katu  ya timu ya Mbezi na makondeko ambapo, timu  hizo zilitoka sare ya bao 2 -2 na kuingia kwenye mkwaju wa penalti ambapo timu ya kawe iliibuka na ushindi wa mabao 7 -6  .
Katika michuano hiyo iliyodumu kwa muda wa juma moja  na kushirikisha timu nane kutoka katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni timu ya  mikocheni  Iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo.
 
Akiongea wakati wa kufunga michuano hiyo mgeni rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh. Pereira Silima alisema” anawashukuru waandalizi wa michuano hii na wadhamini ambao ni Airtel, Mr price, home shoping center na Rotary Club Dar es Saalam kwa ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika kuhakikiksha mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio.  
 
Hii nijitahada ya pekee kuunganisha michezo na elimu ya usalama barabarani. Tumegundua vipaji vingi hapa tunawaasa wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha  pikipiki kwa muda wa ziada wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato kwa michezo ni ajira.
 
Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga amewashukuru washiriki wote wa michuano hii na kusisitiza  wananchi na watanzania kwa ujumla kutii sheria bila shurutishi.
Akiongea kwa niaba ya wadhamini Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” mashindano haya yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa washiriki na wadau wa michezo zaidi tumeshuhudia jinsi mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yalivyoendesha na kuelimisha watumiaji wa barabara waliokuwa wakihudhuria hapa. 
 
Tunaamini kuendelea na  juhudi hizi tutaweza kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea kushirikiana na jeshi la  polisi  usalama barabarani katika shughuli mbalimbali za uelimishaji umma juu ya sheria za barabarani
Michuano ya mpinga cup kwa wilaya ya kinondoni imefika tamati hapo jana na mpango ni kuwa na michuano hii pia katika mkoa wa ilala na temeke na kisha kuendelea na michuano hii nchini nzima.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers