HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 March 2013

RAHMA AL KHAROUZ ATAWEZA MASHARTI HAYA KWA MASHABIKI WA SIMBA AMBAO WAO WANAJUA SULUHU NA KUSHINDA MECHI KUFUNGWA HAWAKUTAMBUI ?


Bibi Hindu ambaye ni mwanachama wa Simba tawi la mpira pesa akiwa na malkia wa nyuki ndani ya ofisi za mpira pesa Magomeni leo usiku. Malkia amekwenda kutafuta suluhu








Malkia wa nyuki usiku wa leo amefika kwennye tawi la mpira pesa lililoko Magomeni Mikumi kwa ajili ya kutafuta suhulu ya mgogoro uliopo kati yao na uongozi wa Simba.

Malkia wa nyuki kwenye kikao hicho alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba na wanachama wa tawi hilo walimpa masharti kadhaa baada ya kukaa kikao kilichochukua takribani saa tatu.

Moja ya masharti aliyopewa ni kuwa uongozi wa Simba ulilifuta tawi hilo kwa kuwapa barua na kutangaza kwenye vyombo vya habari hivyo wanataka taratibu zilizotumika kulifuta zitumike kulirudisha tena.

Pili wametaka uitishwe mkutano Marchi 17 kwa ajili ya kutafuta mstakabali wa klabu ya Simba katika kufanikisha kumalizia michezo nane ya ligi kuu iliyobakia.

Tatu tawi hilo linamtaka Mwenyekiti Ismail Rage na yeye ajiuzulu kama walivyofanya akina Kaburu.

Kikao hicho kilifanyika kwa utulivu na kukubaliana kamati ya utendaji ya Simba inakwenda kukaa na kuyafanyia kazi ili wajenge Simba upya. 
pallagyor.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers