HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 April 2013

TIMU YA TAIFA YA TANZANIA YATAFUTA NAFASI YA KWENDA UHISPANIA KUPITIA ZAMBIA



Timu ya taifa ya kuogelea inaanza harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu kushiriki kwenye michuano ya dunia itakayofanyika Agosti mjini Barcelona, Hispania kwa kutupa karata yake katika michuano ya awali mjini Lusaka, Zambia leo.
Kikosi cha waogeleaji 18 na kocha mmoja kiliondoka jana asubuhi jijini Dar es Salaam kwenda Lusaka tayari kwa michuano ya Afrika inayoanza asubuhi ya leo nchini humo.
Nahodha wa timu hiyo, Hilal Hilal alisema jana kabla ya kuondoka Dar es Salaam kuwa wanakwenda kushinda na si kushiriki na akasisitiza kwamba licha ya timu yao kuwa na rekodi ya kufanya vibaya kwenye michezo ya Olimpiki na Afrika wana mategemeo ya kutwaa medali kwenye michuano hiyo.
"Tumefanya mazoezi ya kutosha chini ya kocha John (Belela), tunategemea hatutamwangusha na pia tutaitangaza vyema nchi yetu kwa kutwaa medali," alisema Hilal.
Kocha wa timu hiyo, Belela alisema wana mategemeo makubwa ya kushinda japo timu za Afrika Kusini na Zimbambwe zinawapa presha kwakuwa nchi hizo zina miundombinu bora ya mchezo huo kulinganisha na Tanzania. 
Belela alisema mbali na mataifa hayo, hakuna nchi nyingine wanayoihofia na kwamba timu yake itafanya vizuri kwa kurejea na medali na pia kufuzu kushiriki mashindano ya dunia.
Kwa mujibu wa mkuu wa msafara wa timu hiyo ambaye pia ni katibu mkuu msaidizi wa chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhani Namkoveka, jumla ya nchi 17 zitashiriki kwenye michuano hiyo.
Namkoveka alizitaja nchi hizo kuwa ni Botswana, Zimbabwe, Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Madagascar, Shelisheli, Angola, Namibia na wenyeji Zambia.
Aidha, aliwashukuru wadhamini wa timu hiyo ya taifa Bay Port Finance Services na MarryBrown kwa kusaidia kufanikisha safari hiyo.
Wachezaji walioondoka ni pamoja na Hilal Hilal, Adam David, Sonia Tumiotto, Sakura Ito, Amaar Ghadiyali, Iyas Shivji, Malindi Vaughan, Anjani Taylor, Matthew Guild, Emma Imhoff, Sabrina Kassam, Mubanga Peeperkorn, Mariam Foum, Mohamed Said, Alizee Bollen, Shammrad Magesvaran, Smriti Gokarm, Dhashrrad Magesvaran na Catherine Mason.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers