HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 May 2013

AFISA WA CHAMA SOKA AFRIKA KUSINI AIBIWA SIMU NA MASHABIKI WA TP MAZEMBE LUBUMBASHI


 

Chama cha soka cha Afrika kusini
 (SAFA) kina tarajia kupeleka malalamiko yake katika shirikisho la soka bara afrika  (CAF) baada ya kuhudumiwa vibaya kimapokezi katika mechi yao ya ligi ya mabingwa barani afrika kati ya Orlando Pirates FC dhidi ya  TP Mazembe FC ya Jamhuri ya Kidemocracia ya watu wa kongo kwenye  mchezo ulichezwa  Lubumbashi jumapili   5 May 2013.
Pirates ilifungwa goli moja kwa bila lakini ilifuzu kwenye hatua inayofuata baada ya ushindi wa mabao matatu kwa mawili mechi ya kwanza ilishinda mabao matatu kwa moja   3-1 kule  Johannesburg majuma mawili yaliyopita .
"Lilikuwa tukio la kukumbukwa . Maisha yetu yalikuwa Hatarini," alisema mkuu wa msafara wa SAFA's , Mr Elvis Shishana, ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa  SAFA (NEC).
Timu ya matangazo ya moja kwa moja ya kituo cha runinga cha  SABC kilikataliwa kurusha mechi kwa kile kilichosemwa kuwa hakukuwa na haki za urushwaji wa mechi hiyo

"Hii ni wazi tangu mwanzo walikuwa na jambo la siri hawa, Na hawakutaka mtu yoyote kunakiri mechi kwenye runinga . nashangaa na ni vigumu kuamini mamilioni ya watu walinyimwa haki ya kutazama mechi hiyo .
"Hata uchezeshaji haukuwa mzuri na tulikuwa tunapoteza, tungekuwa tunaambiwa tunalia kama watoto lakini sasa tumefuzu hatua inayofuata , Lazima tulalamike  CAF," Hili jambo la kuhuzunisha  anasema  Shishana.
Shishana aliongeza japokuwa tulifanyiwa matukio mabaya,lakini wachezaji wa Pirates walifanya kile ambacho Nchi Iliwatuma .
"Vijana wamefanya makubwa kulingana na maisha yao. , Nina jivunia kuwa na vijana hawa wamepita katika wakati mgumu . Na tunafurahi tumerudi nyumbani salama la zima niseme ilikuwa hatari na hari mbaya zaidi ," Shishana ambaye simu yake iliibiwa na shabiki aliyekuwemo kiwanjani, Maaskari walishindwa kumkamata mtuhumiwa hadi pale alipotishia kulipoti swala hilo  CAF.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers